Kinana atwishwa matatizo ya Rorya


WANACHAMA wa Chama Cha mapinduzi wilaya Rorya wamemtwisha makamu mwenyekiti wa Chama hicho Tanzania Bara,AbdulRahman Kinana msalaba wa Watu ambao wanapitapita wakifanya kampeni kabla ya mda kufikia ili kuushugulikia na kuutatua.

Akiongea mwenyekiti wa Chama Cha mapinduzi wilaya Rorya,Ongujo Wakibara maarufu( OWAN) Leo alisema Kwa ujumla Jimbo hilo liko salama kisiasa na hakuna wapinzani kutoka vyama pinzani vya siasa badala yake Jimbo la Rorya linakabiliwa na baadhi ya Watu ambao wanapita wakifanya kampeni kabla ya mda wake.

"Rorya tuko vizuri tunapoelekea kipindi Cha uchaguzi wa serikali za mitaa tutashinda Kwa sababu hatuna upinzani kutoka vyama vya upinzani ila upo upinzani Kwa baadhi ya Watu wakupita pita wakifanya kampeni kabla ya mda wake tunaomba  hilo kulishugulikia na kulitatua"alisema Ongujo.
 
Aidha mwenyekiti huyo alitumia nafasi hiyo kupongeza mwenyekiti wa Chama Cha mapinduzi Taifa na Rais wa jamujuri ya muungano wa Tanzania,DK Samia Suluhu Hassani Kwa kusimamia utekelezaji wa Ilani ya Chama Cha Mapinduzi 2020-2025 na kuwaletea wananchi maendeleo.

Mwenyekiti huyo alimaliza Kwa kuwakaribisha wadau wote wapenda maendeleo kuja Rorya na kuchangia shughuli za maendeleo Kwa utaratibu unaokubalika kichama sii vinginevyo,na kuwa mwenyekiti huyo amefanya ziara ya kuzungukia vijiji vyote huku akitoa misaada kuunga mkono juhudi serikali.

Kwa upande wake Mbunge wa Jimbo la Rorya,Jafari Chege alisema walipoingia madarakani 2020 walikabidhiwa Ilani ya uchaguzi ambapo sasa ametekeleza Kwa kuwapatia maji Watu wa Rorya hususani Shirati wanakunywa maji safi na miradi mbalimbali ametekeleza.

Pia Mbunge huyo alibainisha kuwa furaha yake ni kuona serikali inaenda kutekeleza mradi mikubwa wa Maji kutoka Ziwa Victoria wenye jumla ya zaidi ya shilingi Bilioni 134 na kunufaisha wakazi wa Tarime na Rorya.

Chege alitumia nafasi hiyo kuwaombea wananchi wake barabara ya kiwango Cha lami kutoka Utegi Shirati hadi Kirongwe ili kuinua frusa za kiuchumi na kuuunganisha ujirani mwema Tanzania na Kenya.

Naye Diwani kata ya Goribe,Joseph Ogaja aliwaondoa hofu viongozi ambao wapo madarakani na kuwataka kuacha kukumbatia baadhi ya viongozi jambo ambalo linaendekeza kuwepo makundi.


Makamu mwenyekiti wa Chama Cha mapinduzi Tanzania Baraza.AbdulRahman Kinana alisema Katika kikao Cha pamoja kilichokalia ukumbi wa OWAN uliopo Shirati kuwa maombi yote atayabeba na ataenda kuyafanyia kazi Cha Msingi ni wanachama  kuungana pamoja ili kuwatumikia wananchi ambao wamewachagua.

Kinana alimaliza Kwa kuwaonya Watu wa Rorya kuacha ukabila na kujifunza umoja kutoka kwa mwaasisi Baba wa Taifa mwalimu Julius Kambarage Nyerere ambapo aliunganisha Watanzania kuwa wamoja na sasa Tanzania inasifika kwa Amani Duniani.

Post a Comment

0 Comments