Mati wafunika maadhisho ya Mei mosi Manyara.


John Walter-Babati

Mamia ya Wafanyakazi wa Kampuni ya kuzalisha vinywaji changamshi ya  Mati Super Brands Limited wameshiriki maadhimisho ya siku ya Wafanyakazi ya Mei Mosi yaliyofanyika kimkoa  Katika Viwanja vya Tanzanite Kwaraa mjini Babati Mkoani Manyara na kupambwa na msafara mrefu wa magari ya kusambaza vinywaji kutoka kwenye kampuni hiyo huku Wafanyakazi wakivalia sare ya njano.

Mkurugenzi wa Kamapuni hiyo David Mulokozi amesema kuwa maonyesho  hayo ya magari  yaliyotanguliwa na farasi yanalenga kuonyesha ukubwa wa kampuni hiyo katika kusambaza bidhaa zake za Strong Dry Gin,Tanzanite  Premium Vodka na Sed Pineapple  flavoured  gin.


Mulokozi amesema kuwa kampuni hiyo itaendelea kuwahakikishia wafanyakazi wake Maslahi bora ili waweze kufanya kazi kwa bidii na kuzingatia weledi.


Mkuu wa Wilaya ya Babati Lazaro Twange amesema kuwa serikali itaendelea kuweka mazingira rafiki kwa wafanya kazi ili waweze kutimiza majukumu  yao na kuleta tija mahali pa kazi.


Twange amepongeza  serikali pamoja na sekta binafsi kwa kuwa mstari wa mbele kuajiri na kupunguza changamoto ya ajira nchini.

Post a Comment

0 Comments