Tanzania na Urusi kuimarisha mahusiano.



Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni amesema serikali kupitia wizara imeamua kuunganisha na kuimarisha mahusiano na nchi ya Urusi katika masuala mbalimbali ikiwemo kubadilishana uzoefu sambamba na askari wa vyombo vya ulinzi kwenda nchini Urusi kujifunza njia mbalimbali za kudhibiti uhalifu katika vyuo vilivyopo nchini humo…

Ameyasema hayo wakati wa mazungumzo ya kujadili hatua hizo ambapo amekutana na viongozi watatu kutoka serikali ya Urusi kwa nyakati tofauti akiwemo Katibu wa Baraza la Usalama la Shirikisho la Urusi, Nikolai Patrushev,Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi wa  Serikali ya Urusi,Igor Zubov na Mkuu wa Usalama wa Taifa wa Serikali ya Urusi,Sergey Beseda.



Wakizungumza kwa nyakati tofauti katika vikao hivyo viongozi hao wa serikali ya urusi waliahidi kushirikiana na serikali ya Tanzania katika programu mbalimbali watakazokubaliana ikiwemo udhibiti wa uhalifu wa kimtandao,matishio ya ugaidi na uboreshaji wa teknolojia ya kudhibiti uhalifu wa aina mbalimbali.

Waziri Masauni yupo nchini Russia kuhudhuria Mkutano wa Kimataifa wa Maafisa wa Daraja la Juu kutoka Serikalini wanaohusika na Mambo ya Usalama ambapo mkutano huo unafanyika  katika Jiji la St. Petersburg, ambapo takribani nchi 20 zimehudhuria mkutano huo.

Post a Comment

0 Comments