Twange awataka wananchi watunze misitu kwa manufaa yao.


Na John Walter-Babati

Mkuu wa wilaya ya Babati Lazaro Twange ametoa wito kwa wananchi kuendelea kutunza misitu ili iweze kuleta fursa ya kupata mvua na kuepuka mabadiliko ya tabia nchi.

Ametoa wito huo wakati akizungumza na wananchi wa kata ya Ayalagaya katika mkutano wa hadhara uliofanyika kijiji cha Haysam ambapo wananchi walilamika kuhusu watu wasio waaminifu kuvuna miti katika msitu wa Nowu na kupasua mbao bila kufuata utaratibu.

Katika mkutano huo Twange alisisitiza wananchi kutunza msitu huo kwa nguvu kwa kuwa athari za mabadilikio ya hali ya hewa ikitokea ni wote wataathirika.

"Na bahati mbaya au nzuri mpo karibu na milima, ikikasirika mtatafuta pa kukimbilia, acheni kuharibu misitu"

Aidha, alisema kuwa Serikali kwa kushirikiana na wadau mbalimbali imekuwa ikichukua hatua za kukabiliana na athari zinazotokana na mabadiliko ya tabianchi hivyio amewataka wananchi kuzoea kutumia nishati mbadala ya gesi badala ya kukata miti kwa ajili ya kuni na mkaa ili kulinda misitu.


Post a Comment

0 Comments