Viongozi wa dini Manyara waliombea Taifa.



Na John Walter -Babati

Kuelekea kilele cha miaka 60 ya Muungano viongozi wa dini mbalimbali mkoani Manyara Leo april 26,2024  wameoliombea Taifa, Rais Samia Suluhu na serikali yake ili Tanzania iendelee kuwa na amani, upendo na mshikamano.

Shughuli hiyo iliyofanyika katika uwanja wa Tanzanite Kwaraa mjini Babati ilihudhuriwa na  watumishi wa umma na wananchi wamejitokeza wakimuomba Mungu aendelee kuudumisha  Muungano huo.

Aidha Viongozi hao wa Dini wameiomba Serikali kusikiliza kero mbalimbali zinazowakabili wananchi na kuzifanyia kazi ikiwa ni pamoja na kero za Maji Migogoro ya ardhi, changamoto ambazo zimekuwa sugu katika baadhi ya Maeneo mkoani hapa.

Kwa Upande mwingine wameiomba Serikali kuangalia upya namna ya kuboresha sheria za barabarani na kutoa elimu kwa madereva ili kuzuia ajali zinazoweza kuepukika.



Katika maombi hayo Katibu Tawala wa mkoa wa Manyara Mariam Muhaji ametumia nafasi hiyo kutoa wito kwa viongozi hao wa dini kuendelea kukemea vitendo vya ukatili wa kijinsia ikiwemo ubakaji ambavyo vimekithiri mkoani humo pamoja na wananchi kuwa na hofu ya Mungu.


Post a Comment

0 Comments