Airtel Tanzania yatoa Gawio la faida ya Bilioni 3.9 kwa Wateja wanaotumia huduma za Airtel Money

Airtel Money Tanzania imetangaza kutoa kiasi cha bilioni 3,956,681,813 TZS kama Gawio la Faida la Airtel Money zitakazogawanywa kwa  Wateja na Mawakala wa Airtel Money nchi nzima ambao wamekuwa wakitumia huduma za Airtel Money kati ya Julai hadi Desemba 2023.

Utoaji wa Gawio la Faida ya Airtel Money ni uthibitisho wa kuendela kufanikiwa kwa mikakati ya Airtel money katika kuboresha huduma za kifedha kupitia Airtel Money ili kutoa huduma bora, zenye ubunifu na nafuu kwa wateja. Gawio la Faida la Airtel Money linagawanywa  kwa wateja na Mawakala kuanzia sasa.

Gawio la Faida ya Airtel Money hutolewa kwa wateja na mawakala wa Airtel Money kila robo ya mwaka kulingana kiasi na alichoweka kwenye akaunti yake ya Airtel Money. Kiasi cha gawio anachopata kitawekwa moja kwa moja kwenye akaunti ya Airtel Money.

Wateja wa Airtel Money wataweza kutumia kiasi cha gawio la faida ya Airtel Money wapendavyo ikiwemo  kujinunulia  muda wa maongezi, kutoa kwa wakala au  kulipia bili kama vile DAWASCO, LUKU, na nyinginezo.

Airtel Money ilianza kugawa gawio la faida tangu mwaka 2015 ambapo hadi leo imeshagawa jumla ya bilioni 52 kwa wateja na mawakala wake nchini nzima.  

"Airtel Money Tanzania tutaendea kutekeleza dhamira yetu ya kutoa huduma  nafuu na kuleta mifumo bora ya kupanua  miundombinu ya huduma zetu ili kuendelea kusambaa na kutoa huduma vijijini na mjini,” alisema Andrew Rugamba, Mkurugenzi wa Airtel Money.

Aliongeza "Airtel Money tutaendelea kupanua zaidi mtandao wa mawakala ili kuhakikisha huduma zote za Airtel Money zinapatikana kwa urahisi kwa wananchi walio wengi."

Airtel inajivunia miundombinu yake ya usambazaji ya Airtel Money nchini, ambapo ina zaidi ya Airtel Money Branch 4,000 pamoja na mawakala wa Airtel Money zaidi ya 250,000 nchi nzima. Vilevile, Airtel Tanzania imejiunganisha na mifumo ya malipo kielektroniki, ikiwemo ya serikali ili kuwawezesha wateja kufanya malipo mbalimbali ya serikali wakiwa popote.
 
Airtel Money pia imeunganishwa na zaidi ya benki 40 nchini, hivyo kuwawezesha wateja wa Airtel Money kufanya miamala ya kifedha  kutoka kwenye akaunti zao za benki kwenda kwenye akaunti zao za Airtel Money kwa urahisi, huku wakifurahia kutuma pesa kwa wateja wa Airtel bila gharama yoyote.

Airtel Money Tanzania inaendelea kujizatiti katika kuboresha huduma za kifedha kupitia simu  kwa wateja wake na itandelea kubuni huduma mbambalia kutokana na mahitaji ya wateja wake na watanzania kwa ujumla ili kuendelea kutoa suluhisho la huduma za kifedha kidijitali na kuondoa changamoto ya kutofikiwa na huduma za kifedha popote nchini.

Notes to Editor
About Airtel
Airtel Africa is a leading provider of telecommunications and mobile money services, with a
presence in 14 countries in Africa, primarily in East Africa and Central and West Africa. Airtel
Africa offers an integrated suite of telecoms solutions to its subscribers, including mobile voice and data services as well as mobile money services, both nationally and internationally. We aim to continue providing a simple and intuitive customer experience through streamlined customer journeys.

For more information please contact:
Jackson Mmbando
+255 786 670 120
Jackson.mmbando@airtel.co.tz
OR
Hannah Randa
+255 748 473 648
hannah@p-l.co.ke

Post a Comment

0 Comments