Kamati ya siasa Babati mjini yaridhishwa na utekekezaji miradi ya Maendeleo.


Na John Walter -Babati 

Kamati  ya Siasa ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) wilaya ya Babati mjini chini ya Mwenyekiti wake Elizabeth Malley leo mei 7, 2024 imefanya ziara ya ukaguzi wa miradi ya maendeleo ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa ilani ya Uchaguzi katika Halmashauri ya mji huo kwa mwaka 2020-2025.

Malley amepongeza Menejimenti nzima ya Halmashauri ya Wilaya ya Babati mjini kwa ushirikiano na jitihada za pamoja katika usimamizi wa miradi ya Maendeleo. 

"Mimi niwapongeze sana, Mkuu wa Wilaya, pamoja na Serikali mnafanya kazi nzuri sana" 

Ameridhishwa na miradi ya barabara inayotekelezwa na TARURA kwa usimamizi thabiti wanaofanya kuhakikisha barabara zote ndani ya halmshauri ya mji wa Babati zinapitika pamoja na changomoto iliyopo ya miundombinu kuharibuka kutokana na mvua kubwa.


Naye mkuu wa wilaya ya Babati Lazaro Twange amesema ataendelea kusimamia kikamilifu miradi yote ili wananchi wapate huduma zote za kijamii inavyostahiki.

Miradi iliyotembelewa na Kamati hiyo ni pamoja na ujenzi wa ofisi ya serikali ya mtaa wa Bagara  ziwani wenye zaidi ya shilingi milioni 29,000,000  fedha kutoka mapato ya ndani ya Halmashauri na nguvu za Wananchi ujenzi ukiwa hatua ya umaliziaji.


Mradi wa ujenzi wa matenki mawili ya maji yenye ujazo wa lita milioni 2,000,000  unaotekelezwa na BAWASA wenye thamani ya shilingi Bilioni 2,852,067,721.13  utakaowanifaisha wananchi wa kata za Bagara,Sigino na Maisaka.


Mradi wa ujenzi wa barabara ya Umambe-Malangi na Sawe-Gambush na ujenzi wa boksi kalavati la mriamba,Waka na Hangoni-Mrara katika halmashauri ya mji wa Babati wenye thamani ya shilingi Milioni 441,122,000.


Ujenzi wa  daraja katika mtaa wa Gendi, mradi wa jengo la wagonjwa wa dharura katika hospitali ya mji wa Babati (MRARA) ulioanza kutumika ambao umegharimu shilingi milioni 380,000,000 na jengo la ofisi ya wajasiriamali na maafisa usafirishaji mtaa wa Maisaka uliogharimu fedha za Serikali kuu na mapato ya ndani Milioni 40,000,000.


Post a Comment

0 Comments