RC Manyara aagiza soko jipya Hanang' lianze kutumika.Na John Walter -Hanang'

Mkuu wa mkoa wa Manyara Queen Sendiga ameiagiza Halmashauri ya wilaya ya Hanang'  kukamilisha haraka taratibu zote ili soko jipya lianze kutumiwa na wafanyabiashara.

Aidha,ameagiza shughuli katika soko hilo kuanza mara moja kabla ya siku ya Ijumaa Mei 24, 2024 ili kutoa huduma kwa Wananchi na kuchochea uchumi wa wafanyabiashara, Halmashauri na mkoa kwa ujumla.

Ametoa agizo hilo Leo mei 16,2024 alipofika kukagua soko hilo jipya lililojengwa na serikali baada ya lililokuwa likitumika awali kuharibiwa na maporomoko ya mawe, tope na miti kutoka mlimani Hanang' mwishoni mwa mwaka Jana.

"Mkurugenzi na wataalamu wako hakikisheni mnawahakiki wafanyabiashara pamoja na kukaa kikao na wafanyabiashara wa soko hilo"

Sendiga amesema kikao hicho kitawasaidia wafanyabiashara hao kujua  taratibu za soko hilo na kutatua changamoto zilizopo kabla wafanyabiasha hao kuhamia  katika soko hilo jipya kutoka soko walilokua awali.
Muonekano wa Soko jipya lililojengwa na serikali Katesh wilaya ya Hanang' mkoani Manyara baada ya lililokuwa awali kuharibiwa na maporomoko ya tope,mawe na miti kutoka mlimani Hanang'.

Soko jipya lililojengwa na serikali Katesh wilaya ya Hanang' mkoani Manyara baada ya lililokuwa awali kuharibiwa na maporomoko ya tope,mawe na miti kutoka mlimani Hanang'.


Post a Comment

0 Comments