Wahamiaji haramu 17 wakamatwa mpaka wa Tunduma, Songwe


Na Baraka Messa, Songwe.

IDARA ya uhamiaji mkoa wa Songwe imefanikiwa kuwakamata wahamiaji haramu 17 raia wa Ethiopia wakiwa wamehifadhiwa kwenye nyumba ya msafirishaji katika kata ya mpemba mpaka wa Tunduma wilayani Momba tayari kwa kuvuka kuelekea Nchi za kusaini mwa Afrika .

Kamishna msaidizi wa uhamiaji mkoa wa Songwe Cleth Mumwi amethibitisha kukamatwa kwa wahamiaji hao haramu 17 pamoja na wasafirishaji 7 ambao ni watanzania watano na Warundi wawili juzi mei ,10 mwaka huu 2024 wakiwa katika harakati za kuvuka katika mpaka wa Tunduma.


 amesema wamefanikiwa kuwakamata baada ya kufanya operesheni maalum ya kuwasaka wahamiaji haram  baada ya kuwepo kwa taarifa za kushamiri kwa wahamiaji haram kuingia nchini kupitia mpaka wa Namanga
 
 Aidha Mumwi amesema kuwa raia wa Tanzania waliokamatwa ni wakazi wa mpemba na Tunduma ambao wanadaiwa kutumia mwamvuli wa kufanyabiashara na kilimo .

" Operesheni hii Maalum ilianza rasmi mei, 6,  licha ya kukamatwa wahamiaji 17 na wasafirishaji 7 ambao kati yao ni watanzania watano na Warundi wawili   ,Lakini bado oparesheni hii ni endelevu , tayari tunayo orodha ya watu wengi zaidi wanaohusika na biashara hii haramu" amesema Mumwi.

 ameeleza kuwa hivi karibuni kumekuwepo na kushamiri kwa biashara ya usafirishaji wa wahamiaji haram kwa kutumia magari ambayo huwekwa bendera za vyama na mengine yakiwekwa namba za serikali ili kukwepa mkono wa sheria.

 Kamanda Mumwi amewaonya wote wanaojihusisha na biashara hiyo kuwa wakikamatwa wanaweza kukabiliana na kifungo Cha miaka 20 jela au kulipa fine kiasi Cha shilingi milioni 20.

 Amesema endapo wahamiaji watakutwa katika nyumba basi nyumba hizo zitataifishwa, hivyo kuwataka wanaohusika katika biashara hizo haram kuwataka kutafuta kazi nyingine  zikiwemo biashara nyingine za halali.

Post a Comment

0 Comments