Airtel Tanzania na Unicef wazindua mpango wa Airtel SMARTWASOMI

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akizindua rasmi programu ya Airtel SMARTWASOMI unaosimamiwa na Kampuni ya Airtel Tanzania kwa kushikiana na UNICEF kupitia Wizara elimu

NA REBECA DUWE TANGA

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amezindua rasmi mpango wa Airtel SMARTWASOMI unaosimamiwa na Kampuni ya Airtel Tanzania kwa kushikiana na UNICEF kupitia Wizara elimu ambao utaziunganisha shule za sekondari 3000 ndani ya muda wa miaka mitano na kusaidia wanafunzi kufujinza kwa njia ya tehama.

Mpango huo ambao unalenga kuhakikisha shule hizo zinaweza kusoma bure maudhui ya kidijitali yaliopo kwenye maktaba mtandao ya taasisi ya elimu kupitia internet ya 4G ambapo kwa mwaka huu utaanza na shule 1000.

Akizungumza leo Juni 1, 2024 kwenye maonesho ya  kitaifa ya Sayansi Teknolojia na ubunifu yaliyofanyika katika viwanja vya shule ya Popatlali jijinj Tanga Waziri Mkuu Majaliwa aliipongeza kampuni ya Aitel Tanzania na Unicef kwa kuja na mpango  huo wa SmartWasomi ambao utaleta manufaa makubwa katika jamii.


Kwa upande wake Mkurugunzi  Mkuu wa Taasisi ya Elimu Tanzania (TET) Dkt. Annet Komba amesema Wizara ya Elimu ikishirikiana na Unicef pamoja na Airtel Tanzania pia imeandaa majukwaa  makuu mawili ya kidijitali ambayo yatasaidia kuimarisha matumizi ya tehama katika kufundisha na ujifunzaji.

Dkt. Komba ameongeza kuwa majukwaa hayo pia yamepatiwa maudhui mbalimbali yakiwemo vitabu vya kiada, mtaala ulioboreshwa na mtaala ambao utaendeleea kuukamilishwa.


Nae Mkurugenzi Mtendaji wa Airtel Tanzania, Bw. Dinesh Balsingh alisema kuwa lengo kuu ni kuimarisha matumizi ya tehama katika ufundishaji na ujifunzaji hususani kwa vijana wanaosoma mashulenj na vyuoni kwani matumizi ya internet yakuwa rahisi.

 


Post a Comment

0 Comments