LINDI: DC Ndemanga awataka viongozi waletekeleza kwa weledi mpango jumuishi wa wahudumu wa afya.

 


Na Ahmad Mmow, Lindi.


Viongozi na watendaji mkoani Lindi wametakiwa kuwa na weledi katika kutekeleza mpango jumuishi wa wahudumu wa afya kwa ngazi ya jamii mkoani humo.


Agizo hilo kwa viongozi na watendaji  limetolewa leo tarehe 10.06.2024 mjini Lindi na mkuu wa wilaya ya Lindi, Shaibu Ndemanga ambae alimwakilisha mkuu wa mkoa wa Lindi, Zainab Telack wakati wa utambulisho wa mpango jumuishi wa wahudumu wa afya ngazi ya jamii uliofanyika katika ukumbi wa chuo cha uuguzi Lindi. Ambao pia na ulihudhuriwa na viongozi wa Wilaya na Mkoa .


“Niwakumbushe mambo mawili ya msingi, moja tunapaswa kuwa na weledi katika utekelezaji wa mpango huu, kwani yapo mambo mengi ambayo yanaweza kuibuka wakati wa utekelezaji, hasa katika zoezi la kuchagua watoa huduma ambao kimsingi wanachaguliwa na wanajamii wenyewe , "  Ndemanga alisisitiza.


Mkuu huyo wa wilaya ya Lindi alitumia 

 fursa hiyo kuwakumbusha wataalamu wa ngazi ya wilaya na mkoa kuhusu  umuhimu wa kutunza kumbukumbu ambaz zinasaidia kuondoa sintofahamu wakati wa utekelezaji na baada ya utekelezaji wa kuwapata watoa huduma ngazi ya jamii na shughuli zingine muhimu za kiutendaji.


Alisema hana shaka yoyote kuhusu viongozi na watendaji kufahamu  umuhimu wa kumbukumbu. Kwahiyo katika zoezi hilo wanapaswa kuzingatia uwekaji kumbukumbu sawa kama ambavyo mazoezi mengine yalivyofanyika vizuri.


Kwa upande wake Bi. Orsolina Tolage  ambaye ni Afisa progamu wa mpango wa Huduma za Afya ngazi ya jamii kutoka Wizara ya Afya Idara ya Kinga, Sehemu ya Elimu ya Afya Kwa Umma alieleza  malengo ya mpango huo pamoja na kuzuia magonjwa yasiyo ambukiza kama vile Malaria, Magonjwa yanayotokana na ukosefu wa lishe bora pamoja na magonjwa yanayotokana na mabadiliko ya tabia ya nchi. 


Na ofisa Maendeleo ya Jamii idara ya Serikali za Mitaa Ofisi ya Rais –TAMISEMI Ndugu Jeremiah Mwambange akieleza muongozo wa utaratibu wa kuwapata wahudumu wa Afya ngazi ya jamii alisema kuwa, jamii ndiyo yenye jukumu la kumchagua mhudumu wa Afya ngazi ya jamii kadri itakavyoona inafaa ili kutoa huduma kwa kuzingatia vigezo vilivyowekwa .


Serikali imeweka utaratibu wa kuwapa mafunzo ya kuwajengea uwezo wahudumu tajwa kupitia vyuo vya Afya vya kati na hatimaye kuwawezesha kutekeleza majukumu ngazi ya jamii kwa kuwapa vitendea kazi na motisha.

Post a Comment

0 Comments