Mbunge Rahhi agawa kuku 6,000 kwa Wananchi Mbulu vijijini.


Mbunge wa viti maalum mkoa wa Manyara Mheshimiwa Yustina Rahhi ameendelea kuwawezesha wananchi kwa kuwapatia elimu ya ujasiriamali na kuwapatia mtaji wa kuku wa kufuga.

Akizungumza wakati akifunga mafunzo ya ujasiriamali mheshimiwa Rahhi amewasisitiza wananchi kuhakikisha wanatumia maarifa waliopatiwa ili kujikwamua kiuchumi pamoja na  familia zao.

Aidha amegawa kuku 6,000 kwa vijana na Wanawake wa Halmshauri ya wilaya ya Mbulu walionufaika na Mafunzo ya ujasiriamali wa aina mbalimbali.

Katika hatua nyingine Mheshimiwa Rahhi amewataka wananchi kuchangamkia fursa ya mikopo inayotolewa na serikali kupitia halmashauri zao bila riba. 

Mheshimiwa Rahhi amewasisitiza Wananchi kuendelea kumuombea Raisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt Samia Suluhu Hassan aendelee kuwa na afya njema ili azidi kuwaletea maendele.

Post a Comment

0 Comments