RC Sendiga aagiza taa mbovu zirekebishwe ndani ya siku 14.


Na John Walter -Manyara

Mkuu wa mkoa wa Manyara Mheshimiwa Queen Sendiga ameziagiza TANROADS na TARURA Mkoani humo kurekebisha taa zote mbovu ndani ya siku 14 ili wananchi waweze kupata mwanga nyakati za usiku.

Ametoa agizo hilo leo juni 27, 2024  wakati akiongoza kikao cha pili cha mwaka 2023/24 cha bodi ya barabara Mkoa wa Manyara kilichofanyika ukumbi wa mikutano ambacho chenye kililenga kujadili hoja mbalimbali katika sekta ya hiyo Viongozi mbalimbali wa Serikali, Chama na Taasisi wakihudhuria.

"Taa hizo zilizoharibika, TANROAD na TARURA simamieni ziwake ndani ya siku 14" alisema Sendiga

Aidha Sendiga ameziagiza taasisi hizo kufanya usafi wa mazingira katika mitaro ya barabara pamoja na kuweka alama za barabarani katika maeneo yote yanatostahili.

Mitaa mbalimbali ya mji wa Babati taa zilizopo haziwaki na zingine zimeharibika kutokana na ajali za barabarani.

Post a Comment

0 Comments