Shule zinazopakia Wanafunzi kupita kiasi zaonywa.Na John Walter -Manyara

Madereva na wamiliki wa Magari yanayobeba Wanafunzi wametahadharishwa kubeba Idadi ya watoto kulingana na gari husika.

Angalizo hilo lometolewa na jeshi la polisi kikosi cha usalama barabarani mkoa wa Manyara wakati wakiwa kwenye zoezi la ukaguzi wa Magari yanayobeba Wanafunzi kwenda shuleni na kurudi nyumbani.

"Kuna tatizo kubwa sana baadhi ya shule kubeba watoto wengi kupita uwezo wa gari,hilo tunaendelea kuwahimiza kila kukicha ,mbebe watoto kulingana na uwezo wa gari husika ili kuepuka madhara yanayoweza kutokea pindi inapotokea ajali" alisema Kandola

Jeshi hilo limefanya ukaguzi wa magari ya kubeba wanafunzi (school bus) katika kipindi hiki cha likizo ili kuhakikisha magari hayo hayatembei yakiwa mabovu pindi shule zitakapofunguliwa.

Akizungumza wakati wa zoezi hilo la ukaguzi Kaimu mkuu wa usalama barabarani mkoa wa Manyara Mrakibu msaidizi wa polisi (ACP) Emmanuel Kandolla amesema kuwa wamefanya ukaguzi huo ili kuhakikisha magari hayo yanakua salama wakati wote yanapobeba  wanafunzi na wanafanya hivyo mkoa mzima.


Zoezi hilo la ukaguzi wa magari linakwenda sambamba na utoaji elimu ya usalama barabarani kwa madereva.

Aidha jeshi hilo limewatahadharisha madereva wanaopakia Wanafunzi wengi kupita uwezo wa gari.


Kandola  amesema kuwa madereva wanatakiwa kushirikiana na waajiri wao kufanya ukaguzi wa mara kwa kwenye magari ili kuwa salama muda wote.

Jeshi la Polisi mkoani hapa linaendelea na ukaguzi huo katika wilaya zote.


Post a Comment

0 Comments