Sillo: Lazima tuseme mazuri ya Rais Samia.


Na John Walter -Babati

Mbunge wa Jimbo la Babati vijijini-Naibu waziri wa Mambo ya ndani ya nchi, Mheshimiwa Daniel Sillo akiwa katika  ziara yake ya kibunge kusikiliza kero za wananchi kata ya Kiru amesema katika kipindi cha miaka mitatu ya uongozi wa Rais Dkt Samia Suluhu Hassan yamefanyika mambo makubwa katika kila sekta.

Katika sekta ya elimu, Jimbo hilo  limepata fedha zilizowezesha kujengwa Madarasa 136 shule za Sekondari, shule mpya mbili za Sekondari, Madarasa 52 shule za msingi na maabara 10.

Aidha katika kipindi hicho vimejengwa vituo vipya vya Afya vinne kata za Bashnet, Gidas Madunga, Ayasanda, zahanati tisa pamoja na hospital mpya ya wilaya iliyopo kata ya Mwada.Sillo amewahakikishia Wananchi wa Kiru kuwa serikali ipo kwenye mchakato wa kujenga kituo cha Afya cha kisasa kata ya Kiru ili wananchi wapate huduma Karibu.

Mheshimiwa Sillo ameeleza kwa kipindi cha miaka mitatu pekee serikali imejenga ofisi ya halamshauri ya wilaya ya Baabati kwa shilingi bilioni 3.6.

"Iwe mvua, iwe jua lazima tusimame kusema mambo mazuri ya Maendeleo yanayofanywa na Rais wetu Dkt Samia Suluhu Hassan katika nchi hii" alisisitiza Sillo 


Diwani wa Kata ya Kiru Mheshimiwa Benjamin Keremu ameishukuru Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kupeleka fedha za miradi mbalimbali ya Maendeleo katika kata hiyo hali iliyosaidia kupunguza kero kwa wananchi juu ya michango.

Pamoja na hayo amewakumbusha Wananchi wenye sifa, kujitokeza kugombea nafasi mbalimbali za uongozi katika uchaguzi wa serikali za mitaa hapo baadaye mwaka huu.

Post a Comment

0 Comments