F TAKUKURU Lindi yawataka wananchi wawe majasiri. | Muungwana BLOG
https://c2p.cleverwebserver.com/dashboard/6a0bec4b-79ba-11ef-ad2b-06f0639468d1

TAKUKURU Lindi yawataka wananchi wawe majasiri.

 


Na Ahmad Mmow, Lindi.


Wananchi mkoani Lindi wameaswa wawe majasiri ili kufanikiwa kutokomeza rushwa.


Wito huo ulitolewa jana katika manispaa ya Lindi na mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa(TAKUKURU) wa mkoa wa Lindi,Asha Kwariko wakati wa semina ya siku moja ya wazabuni, walimu na wakandarasi. 


Alisema wanachi wengi wanashindwa kutoa ushirikiano na 

taasisi hiyo kutokana na hofu ya kutengeneza uhasama baina yao na watoaji na wapokeaji rushwa.


Kwakuzingatia ukweli huo Kwariko alisema mapambank dhidi ya rushwa yatashindwa kutoa matokeo chanya iwapo wananchi hawatauvaa ujasiri kwa kufichua vitendo vya rushwa ambavyo ni sawa na sumu katika utoji haki, huduma na maendeleo na uchumi wa nchi.


Amesema sio jambo jema kuona watu wachache wanarudisha nyuma azima ya serikali ya kupeleka ustawi kwa wananchi kwa kupeleka miradi ya maendeleo na huduma za jamii kwa kushindwa kuwafichua kutokana na hofu ya  kutengeneza uhasama.


Kwariko amewataka walimu, wazabuni,wakandarasi watoe taarifa kwa taasisi hiyo pindi wakiombwa rushwa ili miradi iweze kutekelezwa au fedha za kodi ya zuio zikifanyiwa ubadhirifu na kushindwa kupelekwa kwa mamlaka ya mapato(TRA).

Post a Comment

0 Comments