F TRA Lindi yawaonya wamiliki wa vyombo vya moto vya usafiri. | Muungwana BLOG
https://c2p.cleverwebserver.com/dashboard/6a0bec4b-79ba-11ef-ad2b-06f0639468d1

TRA Lindi yawaonya wamiliki wa vyombo vya moto vya usafiri.

 


Na Ahmad Mmow,  Lindi.


Wamiliki wa vyombo vya moto vya usafiri mkoani Lindi wametahadharishwa wasiuze vyombo hivyo au kukatakata wapohisi vimechakaa bila kufuata taratibu zilizopo kwa mujibu wa sheria za nchi.


Tahadhari na wito huo umetolewa leo tarehe 28.07.2024 mjini Lindi na meneja wa mkoa wa Lindi wa mamlaka ya mapato (TRA), Matilda Kunenge kwenye semina ya siku moja  kwa walimu, wakandarasi na wazabuni kuhusu elimu inayohusu kodi.


Alisema vyombo vya moto  vya usafiri vikiwemo pikipiki za tairi mbili, pikipiki za tairi tatu(bajaji) guta na gari vimesajiliwa na kumbu kumbu zake zipo TRA. Kwahiyo kuuziana kinyemela au kukata kwa lengo la kuuza kama vyuma chakavu bila kufuata taratibu na sheria ni kosa ambalo linaweza kuwagharimu.


Alibainisha kwamba baadhi ya wamiliki wakichoka kutumia vyombo wanaamua kuuza bila kufuata taratibu kwa mujibu wa sheria zilizopo na pia wapo wengine ambao wakihisi vyombo vyao vimechakaa wanakatakata bila kufuata taratibu. Huku wakijua kwamba vyombo hivyo vimesajiliwa na kumbukumbu zake zitaendelea kuonesha kwamba wanaendelea kumiliki.


" Lile gari unalo nunua kwa mtu linajina linalomtambulisha aliye kuuzia kwenye mfumo wa mamlaka ya mapato. Ni mali ya serikali na ina eleweka kwamba gari namba fulani lipo kwa mtu fulani. Kwahiyo hamruhusiwi kuuza au kukata vipande bila kufuata taratibu," Kunenge alionya.


Aliwaasa wamiliki wa vyombo vya moto ambao wanahisi au kuona vyombo vyao vimechakaa wakatoe taarifa katika vituo vya polisi. Kwani jeshi hilo lina ujuzi na weledi wa kuvijua vyombo vilivyo chakaa. Kwahiyo likijiridhisha litawaruhusu kukata na matumizi mengine yanayofaa kutumika vyombo chakavu. Huku wanaotaka kuuza wafuate taribu zilizopo kwa mujibu wa sheria za nchi. 


Alisema iwapo vyombo wanavyouza kinyemela vikipata ajali au kusababisha maafa watafuatwa na kuhojiwa wao sio waliowauzia. Huku pia wale wanao kata bila kufuata taratibu watahesabika bado wanamiliki vyombo hivyo. Kwahiyo wote watalazimika kulipa kodi na tozo nyingine zilizopo kisheria.


Aidha Kunenge aliwaasa wafanya biashara mkoani humu walipe kodi kwa hiari na wasihisi kwamba wanaonewa. Kwani hata watumishi wa mamlaka hiyo wanalipa kodi kama watumishi wengine. Kwahiyo wasiwe wanyonge bali wajione wanatimiza wajibu wao wa msingi kama walipa kodi wengine.


Kwa upande wake mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa(TAKUKURU)wa mkoa wa Lindi, Asha Kwariko. Ambae taasisi hiyo anayoongoza ilishirikishwa kwenye semina hiyo alisema walikubaliana na TRA kwamba TAKUKURU ianze kutoa elimu kuhusu madhara ya rushwa na wajibu wa washiriki hao kushiriki kikamilifu kupambana dhidi ya rushwa.


Alisema katika kutekeleza wajibu wake, taasisi hiyo imefuatilia miradi inayotekelezwa na serikali mkoani humu na kubaini kwamba baadhi ya walimu, wazabuni na wakandarasi wanaotekeleza miradi,hasa ya ujenzi hawalipi kodi ya zuio na hawapeleki fedha mamlaka ya mapato(TRA).


Aliweka wazi kwamba baada ya kutoa elimu wakishindwa kubadilika na kuamua kuendelea kutolipa kodi ya zuio na kutopeleka fedha TRA taasisi hiyo haitasita kuwachukulia hatua za kisheria.

Post a Comment

0 Comments