F UWT wakemea mauaji ya mtoto mwenye ualbino, watoa tamko | Muungwana BLOG
https://c2p.cleverwebserver.com/dashboard/6a0bec4b-79ba-11ef-ad2b-06f0639468d1

UWT wakemea mauaji ya mtoto mwenye ualbino, watoa tamko



JUMUIYA ya UMOJA wa Wanawake Tanzania ( UWT ) limetoa tamko kali kuhusina na mauaji ya mtoto mwenye u albino Asimwe Novart ( 2 ) aliyeibiwa nyumbani kwako mnamo Mei 30, 2024.

Akiongea na chombo hiki Cha habari Jana Katibu Mkuu wa UWT Taifa Suzan Peter Kunambi amesema UWT umepokea kwa masikitiko makubwa taarifa za mauaji ya mtoto aitwaye  Asimwe Novart ( 2)  aliyeibiwa na Watu wasiojulikana  mnamo Mei 30,2024.

Aidha KUNAMBI amesema mtoto huyo alikutwa akiwa amekufa mnamo Juni 17,2024 huku mwili wake ukiwa umekatwa katwa na kutolewa baadhi ya viungo kwenye mwili wake huko katika kitongoji Cha Mbale Kijiji cha Bulamula, Kata ya Kamachumu, Wilaya ya Muleba, Mkoani Kagera.

" UWT inalaani vikali na kukemea matukio ya kikatili na ya kinyama dhidhi ya ndugu zetu wenye ulemavu hapa Nchini kwani yanavunja haki, utu, na heshima ya kibinadamu kama  ilivyoainishwa katika katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya Mwaka 1977, Sheria za Nchi pamoja na Mikataba  ya Haki za Binadamu" amesema Katibu Mkuu UWT Taifa 

Aidha KUNAMBI amefafanua kuwa Kufuatia tukio hilo UWT inatoa wito kwa Serikali  kupitia vyombo vya ulinzi na Usalama kuhakikisha wahusika wanatafutwa , wanakamatwa na kufikishwa mbele ya vyombo vya Sheria.

" Pia jamii itoe ushirikiano kwa kutoa taarifa za watu wote wanaojihusisha na vitendo hivyo ili vyombo vya ulinzi vichukue hatua stahiki, Pia ulinzi shirikishi uendelee viongozi ngazi zote kuanzia kitongoji, Kijiji,mtaa, Kata, Wilaya  na Mkoa ili kuwalinda watu wenye ulemavu" amesema KUNAMBI.

Sambamba na hilo UWT pia inatoa wito kwa jamii kuwa na hofu ya Mwenyezi Mungu na kuachana na vitendo vya Imani za kishirikina zinazopelekea kutoa uhai Kwa watu wasio na hatia.

" Watu wenye ulemavu ni ndugu zetu, Wana haki ya kufurahia maisha yao kama wengine katika jamii" amesema Katibu Mkuu UWT Taifa Suzan Peter Kunambi

Post a Comment

0 Comments