Vyama vya ushirika Manyara vyatoa msaada wa mashuka Hospitali Mkoa.Na John Walter -Manyara
Mwenyekiti wa Chama kikuu cha ushirika Rift valley co operative union (RIVACU) ambaye pia ni Mwenyekiti wa Jukwaa la Maendeleo ya vyama vya ushirika mkoa wa Manyara Yuda Sulle , ameuungana na wanachama wengine kutoa msaada wa mashuka 79 katika hospitali ya rufaa ya mkoa wa Manyara.

Akizungumza wakati ugawaji wa Mashuka hayo, Sulle amesema imekua na utaratibu wa kufanya hivyo mara kwa mara ili kurudisha katika jamii ikiwa na kuunga mkono jitihada mbalimbali za serikali ikiwamo kuboresha Sekta ya Afya nchini.

Wametoa msaada huo ikiwa  ni maadhimisho ya wiki ya ushirika duniani ambayo yanatarajiwa kufanyika kitaifa kuanzia juni 29/2024 hadi julai 07/2024 kwenye viwanja vya Nanenane Ipuli Mkoani Tabora yakiongozwa na kauli mbiu isemayo ushirika hujenga kesho iliyo bora kwa wote.

Kwa upande wa mganga mfawidhi wa hospitali ya rufaa ya mkoa wa Manyara Catherine Magali, amewashukuru Wadau hao kwa msaada huo ambao wameeleza kuwa utaenda kusaidia utoaji huduma katika hospital hiyo.
Jukwaa hilo limeketi kwa siku mbili kujadili masuala mbalimbali ya ushirika, fursa, changamoto na namna ya kuzitataua.

Lengo la Maadhimisho hayo ni kuwapa fursa wana ushirika kutangaza fursa zilizopo kwenye Ushirika pamoja na kupanua wigo wa ubia kati ya wana ushirika na wadau wake kitaifa na Kimataifa pamoja na kutafuta suluhu za changamoto za Ushirika.

Post a Comment

0 Comments