F Ajali ya gari yaua Wanafunzi Babati. | Muungwana BLOG
https://c2p.cleverwebserver.com/dashboard/6a0bec4b-79ba-11ef-ad2b-06f0639468d1

Ajali ya gari yaua Wanafunzi Babati.



Na John Walter-Manyara

Watu wanne wamefariki dunia na wengine 31 wamejeruhiwa baada ya gari aina ya Costa yenye namba za usajili T 187 DXV kugongana na gari la mizigo Scania lenye tela namba RL 5485 katika Kijiji cha Gajal wilaya ya Babati mkoa wa Manyara.

Waliofariki katika ajali hiyo iliyotokea asubuhi leo jumamosi agosti 31,2024 ni Wanafunzi watatu wakike na mmoja ni dereva wa gari hilo.

Gari hilo lililokuwa limebeba Wanafunzi wa shule ya Sekondari Endasaki iliyopo wilaya ya Hanang'  lilikuwa likielekea mkoani Arusha baada ya shule kufungwa.

Kamanda wa polisi mkoa wa Manyara kamishna msaidizi mwandamizi Makarani Ahmed akizungumza katika eneo la tukio, amesema chanzo cha ajali hiyo ni uzembe wa dereva wa gari hilo aina ya Scania aliyehama upande wake bila kuchukua tahadahari.



Makarani amesema majeruhi wa ajali hiyo wamepelekwa katika hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Manyara kwa matibabu huku Watano wakiwa katika hali mbaya (ICU).

Kamanda amewataka madareva na watumia barabara kwa ujumla kuwa waangalifu pindi wanapoendesha ili kuepuka ajali zunazosaabisha vifo vya watu na ulemavu wa kudumu.

Hata hivyo Kamanda amesema dereva huyo raia wa Burundi baada ya kusababisha ajali alikimbia na jitihada za kumtafuta zinaendelea.

Naye diwani wa kata ya Dareda Sabini John amesema eneo hilo la Gajal lenye mlima na mteremko mkali lina historia ya ajali za mara kwa Mara.

Post a Comment

0 Comments