F DC Hanang asisitiza Wananchi kujitokeza kupiga kura. | Muungwana BLOG
https://c2p.cleverwebserver.com/dashboard/6a0bec4b-79ba-11ef-ad2b-06f0639468d1

DC Hanang asisitiza Wananchi kujitokeza kupiga kura.


Na John Walter-Manyara

Kuelekea Uchaguzi wa Serikali za Mitaa Novemba 27,2024, Mkuu wa Wilaya Ya Hanang'  Mkoani Manyara, Almish Hazali, amewasisitiza wananchi kujitokeza kwa wingi kupiga kura ili kupata kiongozi Bora na mwenye nia ya maendeleo.

Ameutoa wito huo wakati aliposhiriki ibada ya Uzinduzi wa Kanisa la Elim Pentekoste Tanzania Kata ya Jorodom Wilayani humo, ambapo amesema ni haki ya kila mwananchi kumchagua  kiongozi ambae anaona ana uwezo wa kuleta mabadiliko chanya katika jamii.

Aidha  Almish amewatoa hofu wakazi wa wilaya ya Hanang'   kuwa uchaguzi huo utafanyika  kwa amani na Utulivu kwani ulinzi na usalamà umezidi kuimarishwa.

"Wilaya Yetu Ya Hanang" Ipo Shwari  naomba wananchi wote wa Hanang Tuwe na amani  maeneo yote, maneno mnayosikia ni Maneno Ya mtaani lakini Serikali Muda wote ipo nanyi" Alisema Almish Hazali 

Baadhi ya wananchi wamekiri kuwa na hofu kutokana na uwepo wa taarifa za hivi karibuni za matukio  ya watoto kutekwa kuwawa na kutolewa figo 

"Tumeona taarifa kwenye vyombo vya habari watoto wanapotea kwa mazingira ya utatanishi, kwa kweli hatuna amani ila kwa sababu mkuu wa wilaya ametuambia kuwa kuna ulinzi, tunaomba uendele  uimarishwe  hasa maeneo yetu hayà ya vijijini"Alisema Selina Sixtbet Mkazi wa wilaya Ya Hanang



Kwa Upande wake Askofu Mkuu wa Kanisa la Elim  pentekoste Tanzania Askofu Peter Konki akizungumza wakati Akiweka wakfu Jengo la  Kanisa la Elim Pentekoste Jorodom Amewatahadharisha wananchi  dhidi ya viongozi wanawarubuni kwa zawadi ili wawaingize madarakani.

"Kuuza Kura ni Kujinyima haki ya msingi,Kila mmoja aende apige kura  na kumchagua kuongozi sahihi,kura ni Maamuzi kuuza kura ni kijinyima maamuzi na kuweka kichwa chako kwenye mfuko wa mwenye Elfu Tano, Jambo hili Halikubaliki"Alisema  Peter Konki  Askofu Mkuu wa kanisà la Elim Pentekoste Tànzania

Post a Comment

0 Comments