Jeshi la kujenga Taifa JKT limetangaza nafasi za mafunzo kwa vijana wa kujitolea kujiunga na mafunzo ya Jeshi hilo huku likitoa rai kwa vijana hao kuwa JKT haitoa ajira wala kuwaunganisha na taasisi nyingine kutapa ajira mara baada ya kuhitimu mafunzo hayo bali mafunzo hayo ni kwa ajili ya kuwajengea uzalendo na stadi za maisha.
Akizungumza na waandishi wa habari kwa niaba ya Mkuu wa Jeshi la kujenga Taifa JKT Meja Jenerali Rajabu Mabele, Kaimu Mkuu wa Tawi la Utawala JKT. Kanali Juma Mrai amesema Mkuu wa JKT Meja Jenerali Rajabu Mabele anawaarifu vijana wote wa kitanzania wa bara na visiwani nafasi za kujiunga na mafunzo ya JKT kwa kujitolea.
Ameongeza kuwa “ utaratibu wa vijana kuomba na hatimaye kuchaguliwa kujiunga na mafunzo hayo unaratibiwa na ofisi za wakuu wa Mkoa na Wilaya ambapo muombaji anaishi” amesema.
Amesema usaili wa vijana hao kujiunga na mafunzo ya JKT utaanza Oktoba mosi mwaka huu kwa mikoa yote ya Tanzania Bara na Visiwani na vijana watakaoteuliwa watatakiwa kuripoti kwenye makambi ya JKT kuanzia tarehe 01/11 hadi tarehe 03/11 mwaka 2024.
Ameongeza kuwa “JKT linapenda kuwaarifu vijana watakaopata fulsa hiyo kuwa JKT halitoi ajira, pia halihusiki kuwatafutia ajira katika asasi, vyombo vya ulinzi na usalama na mashirika mbalimbali ya serikali na yasiyokuwa ya kiserikali” Amesema.
Amesema JKT hutoa mafunzo ambayo yatawasaidia vijana kujiajiri wenyewe mara baada ya kumaliza mkataba wao JKT na likibainisha kuwa sifa za muombaji na maelekezo ya vifaa vinavyotakiwa Kwenda navyo yanapatikana katika tovuti ya JKT ambayo ni www.jkt.go.tz.
Amesema Mkuu wa JKT anawakaribisha vijana wote watakaopata fulsa hiyo kuja kujiunga na vijana wenzao ili kujengewa Uzalando, Umoja wa kitaifa, Stadi za Maisha na utayari wa kulijenga Taifa.
0 Comments