F Sillo: Malezi bora ni msingi wa Taifa bora la kesho.. | Muungwana BLOG
https://c2p.cleverwebserver.com/dashboard/6a0bec4b-79ba-11ef-ad2b-06f0639468d1

Sillo: Malezi bora ni msingi wa Taifa bora la kesho..



Na John Walter -Babati 
Wazazi na walezi nchini wametakiwa kuwalinda na kuwaelea watoto katika malezi mema ili kujenga kizazi bora chenye maadili ambacho kitafuata mila na desturi za Kitanzania.

Hayo yamesemwa na Naibu waziri wa Mambo ya ndani ya nchi Mbunge wa Babati vijijini Mheshimiwa Daniel Sillo wakati akizungumza na wazazi, Wanafunzi na walimu kwenye mahafali ya 15 shule maalum ya msingi Jamii ya kifugaji Birisima iliyopo kijiji cha Gedewar Kata ya Dabil wilaya ya Babati mkoani Manyara leo septemba 18,2024.

Sillo amesema Viongozi bora wa baadaye wanatokana na malezi bora ya sasa hivyo kila mmoja atimize wajibu wake.

Aidha Mh.Sillo ameeleza kuwa matukio yanayotokea maeneo mbalimbali nchini ya ubakaji,ulawiti na mapenzi ya jinsia Moja ni matokeo ya malezi mabaya kutoka kwenye baadhi familia zao.


Katika hafla hiyo Wanafunzi walisema wanachangamoto mbalimbali ikiwemo ukosefu wa barabara nzuri kuelekea shuleni hapo, jambo ambalo Mheshimiwa Sillo ameahidi litashugulikiwa n TARURA kuanzia wiki ijayo.

Shule ya Msingi Birisima ilianza ikiwa na Wanafunzi 55 lakini kwa sasa ina Wanafunzi 720 ikiwa na sifa kufanya vizuri katika mitihani ya darasa la saba.

Post a Comment

0 Comments