F Ibada ya kumuombea baba wa Taifa hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere | Muungwana BLOG
https://c2p.cleverwebserver.com/dashboard/6a0bec4b-79ba-11ef-ad2b-06f0639468d1

Ibada ya kumuombea baba wa Taifa hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango na Mkewe Mama Mbonimpaye Mpango wameungana na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan pamoja na viongozi , waumini na wananchi mbalimbali katika Ibada ya Misa Takatifu ya Kumbukizi ya Baba wa Taifa Hayati Mwalimu. Julius Kambarage Nyerere iliyofanyika katika Kanisa Katoliki Parokia ya Mtakatifu Francis Xavier iliyopo Nyakahoja Jijini Mwanza.
 
Akizungumza kwa niaba ya Rais Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan mara baada ya kumalizika kwa ibada hiyo, Makamu wa Rais amesema serikali inawashukuru viongozi wa dini kwa kuendelea kuliombea Taifa pamoja na Viongozi wake.
 
Makamu wa Rais amesema Baba wa Taifa Hayati Mwl. Julius Kambarage Nyerere ameacha misingi imara inayojenga Taifa imara ambayo viongozi wa sasa na wajao hawana budi kuiendeleza.
 
Ametaja mambo mbalimbali ambayo Baba wa Taifa alitekeleza enzi za uhai wake kama ifuatavyo.
 
✓ Aliongoza kwa ustadi jitihada za kuipatia Tanganyika uhuru na kuunganisha makabila zaidi ya 120 na kuwezesha kutumika kwa lugha moja ya kiswahili. Alibainisha wazi wazi nia yake ya kuchelewesha uhuru wa Tanganyika hadi nchi nyingine ziwe huru. Chini ya uongozi wake, Tanzania ilitoa rasilimali zake kusaidia harakati za ukombozi wa nchi nyingine, Mf. Msumbiji, Angola, Namibia, Afrika Kusini.
✓ Alikuwa Mwanamajui (Pan-Africanist) halisi, aliyeasisi muungano wa Tanganyika na Zanzibar na alikuwa miongoni mwa waasisi wa Umoja wa Nchi huru za Afrika (OAU) kwa lengo la kuwaunganisha Waafrika.
✓ Mwalimu alikuwa mpenda amani. Ametuachia tunu ya amani na kuifanya nchi yetu kuwa kisiwa cha amani. Aidha, alikuwa msuluhishi mahiri wa migogoro ya Mataifa mengi Barani Afrika, mf. Burundi.
✓ Alisimamia ulinzi wa Taifa letu kwa nguvu zote. Kwa mfano, Nduli Idd Amini alipojaribu kukalia kipande cha ardhi yetu, Mwalimu aliwaongoza Watanzania kumfukuza mvamizi huyo na kuwasaidia Waganda kumwondosha kabisa.

Post a Comment

0 Comments