F Bilioni 17 kubeba ujenzi wa stendi kuu na barabara za lami Mjini Babati | Muungwana BLOG
https://c2p.cleverwebserver.com/dashboard/6a0bec4b-79ba-11ef-ad2b-06f0639468d1

Bilioni 17 kubeba ujenzi wa stendi kuu na barabara za lami Mjini Babati

Na John Walter -Babati 

Serikali imetenga Shilingi bilioni 17 kwa ajili ya ujenzi wa Stendi Kuu ya Kisasa mjini Babati pamoja na ujenzi wa kilomita 10 za barabara za lami katika mji huo. 

Ujenzi wa miradi hiyo unatarajiwa kuanza rasmi mwezi Mei 2025 kama sehemu ya kuboresha miundombinu na huduma kwa wananchi.

Mbunge wa Jimbo la Babati Mjini, Mheshimiwa Paulina Gekul, amesema kuwa hiyo ni hatua nyingine muhimu ya maendeleo inayoletwa na Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan.

Amesema kuwa miradi hiyo itaongeza ufanisi wa usafiri, kuboresha uchumi wa eneo hilo, na kuhakikisha wananchi wanapata huduma bora za usafiri wa ndani na nje ya mji wa Babati.

Aidha, Mheshimiwa Gekul amewataka wananchi kuthamini juhudi hizo na kueleza kuwa ifikapo Oktoba 2025, wakati wa Uchaguzi Mkuu, hakutakuwa na sababu ya kuuliza maswali bali ni kuhakikisha Chama Cha Mapinduzi (CCM) kinaendelea kupewa ushindi kuanzia ngazi ya madiwani, wabunge hadi rais.

Wananchi wa Babati wamepokea taarifa hizo kwa furaha, wakiamini kuwa miradi hiyo itakuwa chachu ya maendeleo na kuongeza thamani ya mji huo katika siku zijazo.

Post a Comment

0 Comments