F Bodi ya ithibati kwa Waandishi wa habari yazinduliwa. | Muungwana BLOG
https://c2p.cleverwebserver.com/dashboard/6a0bec4b-79ba-11ef-ad2b-06f0639468d1

Bodi ya ithibati kwa Waandishi wa habari yazinduliwa.


Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Prof. Palamagamba Kabudi leo Machi 3, 2025 jijini Dar es Salaam amezindua Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari (JAB) ambayo itakuwa ikishughulikia masuala ya taaluma ya Waandishi wa Habari.

Uzinduzi huo umehudhuriwa na wadau wa habari wakiwemo Waandishi wa Habari, pamoja na wawakilishi wa taasisi mbalimbali zinazohusika na Sekta ya Habari nchini.

Katika uzinduzi huo Waziri Kabudi amemkabidhi vitendea kazi Mwenyekiti wa Bodi hiyo, Tido Mhando, vinavyojumuisha: Sera ya Habari na Utangazaji ya Mwaka 2003; Sheria ya Huduma za Habari Sura ya 229 pamoja na Kanuni za Sheria ya Huduma za Habari za Mwaka 2017.

Post a Comment

0 Comments