F JWTZ yatangaza Nafasi za kuandikishwa Jeshini kwa Vijana Wenye Taaluma za Tiba na Uhandisi | Muungwana BLOG
https://c2p.cleverwebserver.com/dashboard/6a0bec4b-79ba-11ef-ad2b-06f0639468d1

JWTZ yatangaza Nafasi za kuandikishwa Jeshini kwa Vijana Wenye Taaluma za Tiba na Uhandisi

 



J
eshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) limetangaza nafasi za kuandikishwa Jeshini kwa vijana wa Kitanzania wenye elimu ya taaluma za udaktari bobevu kwenye sekta mbalimbali, uhandisi na ufundi mchundo wa kuanzia elimu ya Sekondari hadi elimu ya juu kwa ajili ya kupatiwa mafunzo na kulitumikia jeshi hapa nchini.

 

Akizungumza na waandishi wa Habari Makao Mkuu ya Jeshi la Ulinzi Jijini Dodoma Kaimu Mkurugenzi wa Habari na Uhusiano (JWTZ) Kanali Gaudentius Ilonda kwa vijana wenye sifa hizo watatakiwa kuanza kutuma maombi yao kuanzania Mei Mosi 2025 hadi Mei 14, 2025 na maombi yatimwe kwa maandishi ya Mkono.

 

Amesema sifa za mwombaji ni lazima awe raia wa Tanzania mwenye kitambulisho cha Taifa, awe na afya timamu, mwenye tabia na nidhamu nzuri, hajapatikana na hatia ya makosa ya jinai mahakamani na kufungwa, Cheti halisi Cha kuzaliwa, Vyeti vya Shule na taaluma.

 

Kanali Ilonda amebainisha kuwa awe hajatumikia Jeshi la Polisi, Magereza,Chuo Cha Mafunzo au kikosi Cha kuzuia Magendo,awe amehitimu Mafunzo ya Jeshi la Kujenga Taifa JKT kwa mkataba wa kujitolea au mujibu wa sheria na kutunukiwa Cheti na JKT.

 



Amesema kwa vijana wenye elimu ya kidato cha Nne na kidato cha Sita wawe na umri usiozidi miaka 24,
Vijana wenye Elimu ya Stashahada umri usiozidi miaka 26, Vijana wenye elimu ya juu umri usiozidi miaka 27, na wenye Taaluma ya Madaktari Bingwa wa binadamu umri usiozidi miaka 35 ya kuzaliwa.

 

Kwa Upande wa Taaluma adimu za Tiba zinazohitajika ni Generall Surgeon,Orthopaedic Surgeon,Urologist Radiologist,ENT Specialist,Anaesthesiologist,Physician, Ophthalmologist, Paediatrician, Obstetrician & Gynaecologist,Ocologis, Pathologist, Psychiatrist, Emergency Medicine Specialist na Haematologist.

 

Pamoja na Medical Doctor, Dental Doctor, Veterinary Medicine,Bio Medical Engineer,Dental Laboratory Technician, Anaesthetic, Radiographer,Optometry, Physiotherapy na Aviation Doctor.

 

Kanali Ilonda amebainisha kuwa kwa Taaluma za Uhandisi ni pamoja na Bachelor of Electronic Engineering, Bachelor of Mechanical Engineering, Bachelor in Marine Engineering, Bachelor in Marine transportation & Nautical Science, Bachelor in Mechanic in Marine Diesel Engine, Bachelor in Aviation Management, Bachelor in Aircraft Accident & Incident Investigation, Bachelor in Meteorology, Air Traffic Management & Aeronautic Engineering bila kusahau Fundi Mchundo Aluminum Welding na Welding & Metal Fabrication.

 

Amesema utaratibu wa kutuma maombi kwa makundi yote mawili ni maombi yote yaandikwe Kwa mkono na yawasilishwe Makao Makuu ya Jeshi Dodoma kuanzia Mei 1 2025 hadi tarehe 14 Mei,2025 yakiwa na Nakala ya kitambulisho cha Taifa au nambari ya NIDA,Nakala ya Cheti Cha kuzaliwa,vyeti vya Shule na chuo, Nakala ya Cheti Cha JKT kwa waombaji waliomaliza mkataba wa kujitolea pamoja na nambari ya simu ya mkononi ya Mwombaji.

 

Hata hivyo ametoa angalizo kwa wananchi kutokubali kurubuniwa na matapeli kwa kudai hatua kali zitachukuliwa kwao ikiwemo kupelekwa Polisi.


 

Post a Comment

0 Comments