F UVCCM Kiromo waazimia kumuunga mkono mgombea Urais Dkt. Samia Suluhu | Muungwana BLOG
https://c2p.cleverwebserver.com/dashboard/6a0bec4b-79ba-11ef-ad2b-06f0639468d1

UVCCM Kiromo waazimia kumuunga mkono mgombea Urais Dkt. Samia Suluhu



Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi kata ya Kilomo wilaya ya Bagamoyo Mkoani Pwani wameadhimia kwa pamoja kumuunga mkono mgombea Urais wa Jamuhuri ya Muungwano wa Tanzania kwa tiketi ya CCM Dkt. Samia Suluhu Hassan.

Azimio hilo limetoa Aprili 13, 2025 katika kikao cha kikanuni cha kujadiliana mstakabali wa Umoja huo katika kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi mkuu wa Oktoba 2025 chini ya mwenyekiti wake CDE Hans Msemwa.

CDE Msemwa amesema kuwa baraza hilo limeridhishwa na utendaji kazi wa Dkt Samia kwa kipindi cha miaka minne ambapo ameonesha umahiri mkubwa katika kusimamia miradi iliyoachwa na Hayati Dkt Magufuli na kubuni miradi mingine mipya ambayo inamanufaa makubwa kwa jamii yetu.

"Vijana tunaamini kuzaa sio kazi, kazi kulea hivyo mama samia ameonesha umahiri mkubwa sana katika kuhakikisha miradi iliyokuwa imeanza utekelezaji wake kipindi cha serikali ya awamu ya tano inakamilika kwa mafanikio makubwa"

Baraza  la vijana lipo tayari kusimama na kumpigania Dkt Samia , kumsemea vizuri na kutangaza mambo makubwa aliyoyafanya katika kipindi cha miaka minne na kuahidi kusimama nae katika kipindi cha kampeni kuelekea uchaguzi mkuu wa 2025.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM kata ya Kiromo Bw, Bushili Hamisi Kitumboi amewaasa vijana hao kukataa kutumika vibaya na wanasiasa bali kumpitisha na kuchagua  mgombea mwenye nia ya dhati ya kuleta maendeleo katika kata ya Kiromo.

Aidha amewataka kujikokeza kuchukua fomu za kuwania nafasi mbalimbali za uchaguzi pale muda wa kuchukua fomu utakapofika.

Naye katibu wa CCM kata ya Kiromo Ndugu  Shabani Simba amesema  Umoja wa vijana si watoto hivyo sio kila mtu anapaswa kuwapangia cha kufanya bila kupima matokeo yake. Pia amewaasa vijana kuacha kuwa na makundi ndani ya chama na badala yake kumuunga mkono mtu atakaepitishwa na chama katika kupeperusha bendera ya chama cha mapinduzi.






 


Post a Comment

0 Comments