Wananchi wa vijiji vya Magazini,Sasawala,Amani na Likusanguse wilayani Namtumbo mkoani Ruvuma wameishukuru serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuona umuhimu wa kuwaletea gari la kubebea wagonjwa katika kituo cha Afya cha Magazini kilichopo umbali wa zaidi ya kilomita 230 kutoka makao makuu ya kata ya Magazini hadi Makao Makuu ya Wilaya ya Namtumbo ambako kuna hospitali ya Serikali ya Wilaya.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti na waandishi wa habari Aprili 22/205 kwenye afla ya kukabidhi gari la kubebea wagonjwa ambalo Mbunge wa Jimbo la Namtumbo Vita Kawawa amelikabidhi kwa wananchi wa kata hiyo wamesema kuwa gari hilo litawasaidia kuokoa maisha ya watu kwa kuwapeleka hospitali kubwa pale inapobidi tofauti na awali wagonjwa walikuwa wakisafirishwa kwa kutumia matenga,baiskeli na pikipiki.
Anold Mbunda Mkazi wa kijiji cha Lingusenguse alisema kuwa walikuwa wanapata adha kubwa kwa wamama wajawazito wanapotaka kwenda hospitali kubwa kwaajiri ya kujifungua wanatembea umbali mrefu zaidi ya kilomita 230 ambako kuna Hospitali ya Serikali.
Mganga mkuu wa Wilaya Dk. Aron Hyela alisema kuwa kituo cha afya cha Magazini kati ya vituo 60 vya kutolea huduma za afya ambacho kipo umbali wa kilomita 230 kutoka makao makuu ya halamashauri ya Wilaya ya Namtumbo.
Dk. Hyera alisema kuwa kituo cha afya cha Magazini kilipokea zaidi y ash. Milioni 500 kwaajiri ya ujenzi wa majengo 5 ambayo ni jengo la Wagonjwa wa nje, Upasuaji,Maabara,Nyumba moja ya Mtumishi,Jengo la wazazi na chumba cha kuhifadhia Maiti ambapo kituo hicho kina jumla ya watumishi 7sawa na asilimia 13 kati ya 53 ya watumishi wanaohitajika kwa ngazi ya kituo cha afya na kina uwezo wa kuhudumia jumla ya watu elfu 13.
Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi wa halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo Jonah Katanga alisema kuwa halmashauri imetekereza miradi mbalimbali katika kata ya Magazini ikiwemo ujenzi wa kituo cha Walimu,Nyumba za Walimu na miradi mingine ya maendeleo yenye lengo la kuboresha huduma za wananchi.
Naye Mbunge wa Jimbo la Namtumbo vita Kawawa amewaomba watumishi wa kituo cha afya cha Magazini kuona umuhimu wa kulitunza gari la kubebea wagonjwa ambalo litaweza kuwasaidia wakazi kata ya magazine pale wanapohitaji kwenda hospitali kubwa kwaajiri ya uchunguzi zaidi na akina amama wajawazito wanaopata rufaa kwenda hospitali kubwa kwaajiri ya kujifungua.
Aidha amewataka kutotumia gari hilo kwa manufaa yao binafsi ikiwemo kubebea mafuta,abiria na bidhaa zingine na kuwaomba wananchi wa kata hiyo kuendelea kumuunga mkono Rais Samia na serikali yake kutokana na juhudi mbalimbali anzofanya za kuwaletea maendeleo ikiwemo kuboresha miundombinu kwenye sekta ya afya .
0 Comments