F Wanasheria waomba kampeni ya msadaa wa kisheria Mama Samia LEGAL AID uwe endelevu | Muungwana BLOG
https://c2p.cleverwebserver.com/dashboard/6a0bec4b-79ba-11ef-ad2b-06f0639468d1

Wanasheria waomba kampeni ya msadaa wa kisheria Mama Samia LEGAL AID uwe endelevu


Na Rebeca Duwe Tanga
 

Baadhi ya wanasheria wanaoendelea kuendesha Kampeni ya Mama Samia LEGAL AID wameiomba Serikali zoezi la masaada wa kisheria liwe endelevu ili kuweza kuwafikia wale wananchi waisiojiweza hususani wazee na wale maeneo y pembezoni.

Hayo aliyasema wakili wa Chama cha wanasheria TLS Tanga Chapter Bi.Neema Burhan wakati aizungumza na waandishi wa habari namna zoezi linavyoendelea ambapo alisema kupitia zoezi hilo migogoro iliyodumu kwa muda mrefu imetatuliwa ndani siku tatu.

Aliongeza kuwa migogoro mingi iiyojitokeza ni pamoja na migogoro ya ardhi ,madai ya ajira ambapo imesababishwa na uelewa mdogo wa wananchi juu ya kupata haki zao.

Kwa upande wake Afisa ardhi wa jiji la Tanga Antelis Englebert alisema migorogoro ardhi mingi iliyojitokeza imetokana wananchi wengi wa Tanga, kutouwa na uelewa wa kutosha juu ya ya historia ya  mabadiliko wa sheria ya ardhi ambapo maeneo mengi yalikiwa na miliki halali ya serikali na mamlaka ya Mkonge hivyo endapo wananchi wakipewa elimu kujua utaratibu migororo itapungua.

Dkt Kulwa Magamba ni mratibu kampeni ya SAMIA LEGAL AID jiji la Tanga ambaye alikuwa na timu ya  jopo la wanasheria waliojichimbia uwandani  alisema kuwa miongoni mwa vitendo vya ukatili waliyokutana nayo ni pamoja na  Ulawiti, vipigo nạ ajira kwa watoto ambapo ni  vitendo vinavyo dhoofisha wanafunzi kielimu nạ kiafya.

Sambamba na hayo  Dkt Kila Gamba alielezea jinsi ambavyo waliweza  kumsadia   mwananchi aliyekuwa anapoteza haki zake katika kesi ambayo upande anao lakamikia wote ni marehemu hilo limetokona uelewa mdogo kwa mwananchi huyo kuwa angeweza kupata lakini baada ya timu hiyo kufika na kumwelewesha kumaliza kabisa mgogoro yake.
 Aliongeza kuwa tayari wameshasikiliza migororo  zaidi ya 600 na migogoro mingine imekwisha kabisa lakini migororo mingi zaidi ni ya ardhi ambayo pia mingine imitokana na uelewa mdogo wa kisheria.


Post a Comment

0 Comments