F Peter Nyalandu akusanya zaidi ya Milioni 24 Kanisani Endasak | Muungwana BLOG
https://c2p.cleverwebserver.com/dashboard/6a0bec4b-79ba-11ef-ad2b-06f0639468d1

Peter Nyalandu akusanya zaidi ya Milioni 24 Kanisani Endasak

Na John Walter -Hanang' 

Katika tukio lililojawa na mshikamano, upendo na uzalendo wa kiroho, Mjumbe wa Kamati ya Siasa ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Hanang', Peter Nyalandu, ameongoza harambee ya kuchangia ujenzi na ukarabati wa Kanisa Katoliki la Parokia ya Endasaki, ambapo zaidi ya shilingi milioni 24 zilichangishwa.

Harambee hiyo, iliyofanyika kwa hamasa kubwa, ilihudhuriwa pia na Waziri Mstaafu na Mbunge wa zamani wa Singida Kaskazini, Lazaro Nyalandu, pamoja na kikundi cha vijana mashuhuri kijulikanacho kama Samia Love, waliounga mkono shughuli hiyo ya kijamii na kiroho.

Peter Nyalandu alitoa mchango wake wa shilingi milioni 6 taslimu, na kuchochea ari ya waumini, wadau, na marafiki wa kanisa hilo kushiriki kwa moyo mmoja. 

Jumla ya shilingi 24,607,300 zilipatikana kupitia njia mbalimbali za uchangishaji, ikiwa ni pamoja na:

  • Shilingi 14,386,250 zilizotolewa kwa fedha taslimu;

  • Shilingi 3,446,000 kuwekwa moja kwa moja katika akaunti ya parokia;

  • Shilingi 6,775,000 kuahidiwa na wachangiaji mbalimbali kwa ajili ya kusaidia kazi hiyo ya kiroho.

Akizungumza baada ya harambee hiyo, Paroko wa Parokia ya Endasaki alitoa shukrani kwa waumini na wadau wote waliojitokeza kushiriki, akisisitiza kuwa fedha hizo zitatumika kwa uwazi na uaminifu kwa ajili ya kuharakisha ukamilishaji wa ujenzi wa nyumba hiyo ya ibada.

“Ni matumaini yetu kuwa hatua hii itakuwa chachu ya maendeleo ya kiroho na kijamii kwa waumini wetu, na tunatoa ahadi ya kuhakikisha matumizi sahihi ya kila senti iliyochangwa,” alisema Paroko huyo kwa furaha.





Post a Comment

0 Comments