F REA yahamasisha Wananchi kuunganisha umeme Njombe | Muungwana BLOG
https://c2p.cleverwebserver.com/dashboard/6a0bec4b-79ba-11ef-ad2b-06f0639468d1

REA yahamasisha Wananchi kuunganisha umeme Njombe


Na John Walter-Njombe 

Wakala wa Nishati Vijijini REA imetembelea vitongoji  vilivyopo Makambako mkoani Njombe kwa lengo la kutoa elimu na kuhamasisha umma kuunganisha umeme.

Wananchi hao wameonesha dhamira ya kupokea mradi  ambao unaendelea kutekelezwa katika Mkoa wa Njombe ambako jumla ya wateja 2,970 watanufaika kupitia Mradi wa kusambaza Umeme katika Vitongoji (HEP 2A ) wenye gharama ya Shilingi bilioni 10 kwa kufanya wiring katika nyumba zao.

Akizungumza na wananchi wa vitongoji vinne vya Kijiji Cha Mtulingala, Mbugani  na Nyamande A,  Meneja wa Wakala wa Nishati Vijijini mkoa wa Njombe Mhandisi Marlon  Bulugu amewataka wananchi hao kufanya maandalizi ya kuunganisha umeme katika nyumba zao kwa kufanya wiring na kuwaeleza kuwa  gharama za kuunganisha umeme katika miradi ya REA ni Tsh. 27,000/- tu.

Akielezea kuhusu huduma ya kuunganishiwa Umeme, Afisa Maendeleo ya Jamii wa REA, Bi Jaina Msuya, amewataka wananchi hao kutumia mafundi maalumu waliosajiliwa na EWURA ili kuepuka matapeli na adha mbalimbali zinazoweza kujitokeza.

Kupitia mikutano hiyo ya kutoa elimu kwa umma, wananchi walifundishwa  namna ya kufanya maombi ya Umeme kupitia simu za mkononi.

Wakiishukuru REA kwa nyakati tofauti, wananchi wa vijiji hivyo, Ndugu Julius Benard Msigwa na Fidelis Kalili wakazi wa Kitongoji cha Nyamande A wamesema, wanashukuru kwa kupatiwa elimu hiyo na wataweza kuepuka vishoka na kupoteza fedha zao.

Aidha, wananchi hao wamemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuwaletea miradi mbalimbali ya umeme kwa bei ruzuku hivyo kuwawezesha  kuunganisha Umeme kwa gharama nafuu.

Picha mbalimbali za uhamasishaji.














Post a Comment

0 Comments