F Aliyekuwa DED Mvomero achukua fomu ya Ubunge viti maalum Manyara | Muungwana BLOG

Aliyekuwa DED Mvomero achukua fomu ya Ubunge viti maalum Manyara



Na John Walter -Babati 

Aliyekuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mvomero mkoani Morogoro, Loema Peter, leo amechukua rasmi fomu ya kuwania Ubunge wa Viti Maalum Mkoa wa Manyara kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Tukio hilo limefanyika katika ofisi za Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) Mkoa wa Manyara, ambapo Loema amekabidhiwa fomu na Katibu wa UWT mkoa huo, Ndg. Anjela Milembe.

Loema Peter, ambaye ni mzaliwa wa Mkoa wa Manyara, pia ni mmiliki wa shule ya Think Big Pre and Primary School iliyopo Wilaya ya Babati, Manyara.

Akizungumza mara baada ya kuchukua fomu, Loema amesema ameamua kuomba ridhaa ya wananchi ili kuendelea kutoa mchango wake katika maendeleo ya mkoa huo na taifa kwa ujumla.

Uchaguzi Mkuu wa mwaka huu unatarajiwa kufanyika Oktoba 25, 2025.

Post a Comment

0 Comments