Na John Walter -Babati
Katika jitihada za kuimarisha ushirikiano na makundi mbalimbali ya kijamii, Kampuni ya vinywaji changamshi Mati Super Brands LTD imeendelea kutambua na kuthamini mchango wa vijana wanaotangaza bidhaa zake kupitia vyombo vya usafiri, hususan bajaji katika mji wa Babati.
Vijana wawili, Idd Mbwambo na Jonathan Elisa, waliobandika picha za bidhaa mbalimbali za Mati Super Brands kwenye bajaji zao, wamepokea motisha maalum kutoka kwa kampuni hiyo, ambapo wamelipiwa gharama zote za mwezi mzima kwa mabosi zao.
Hali hiyo imewawezesha vijana hao kutumia muda wao kwa sasa kujitafutia kipato kwa ajili ya kujikimu kimaisha. 

Wakiwa na furaha, vijana hao wameeleza kuwa wataendelea kuwa mabalozi wa hiari wa bidhaa za Mati Super Brands, wakisifia moyo wa mkurugenzi wa kampuni hiyo, David Damian Mulokozi, kwa kujitoa kusaidia vijana kiuchumi kupitia ajira zaidi ya 300 alizozitoa.
“Tuna ndoto ya kukutana na Mkurugenzi Mulokozi, hata kupiga naye picha. Ni mtu mwenye moyo wa tofauti sana,” alisema mmoja wa vijana hao kwa furaha.
Kwa upande wake, Brand Meneja wa Kampuni hiyo, Isaack Piganio, amesema kuwa kampuni itaendelea kutoa zawadi na motisha kwa wale wote wanaoendelea kusapoti bidhaa za Mati Super Brands kupitia magari, pikipiki, bajaji na maeneo mengine ya wazi.
Naye Afisa Masoko wa kampuni hiyo, Gwandume Mpome, amesisitiza kuwa msaada wa kampuni hiyo utaendelea kutolewa kwa wale wote wanaojitolea kuisapoti kampuni katika sekta mbalimbali kama michezo, burudani na shughuli za kijamii.
Miezi michache iliyopita, Mkurugenzi wa Mati Super Brands LTD, David Damian Mulokozi, alizindua rasmi “challenge” ya kuwazawadia wote wanaobandika picha za bidhaa za kampuni hiyo kwenye vyombo vyao vya usafiri.
Hii ni baada ya kijana Abdul kuibuka mshindi na kupewa bajaji mpya, baada ya kuonekana kupitia Walter Habari akiwa amebandika picha ya Strong Dry Gin kwenye bajaji yake.
Kupitia jitihada hizi, Mati Super Brands LTD inaendelea kujikita si tu katika biashara ya vinywaji, bali pia katika kuleta mabadiliko chanya ya kijamii kwa kuwahusisha na kuwawezesha vijana wa Kitanzania.
0 Comments