Na John Walter -Babati
Leo Juni 29, 2025, Phabiola Bohay amejitokeza kuchukua fomu ya kugombea Ubunge wa Viti Maalum Mkoa wa Manyara kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM).
Fomu hiyo imekabidhiwa rasmi kwake na Katibu wa UWT Mkoa wa Manyara, Bi. Anjela Milembe, ambaye amesema kuwa zoezi la utoaji wa fomu linaendelea vizuri.
Katibu huyo amebainisha kuwa hadi sasa wanawake zaidi ya sita tayari wamejitokeza kuchukua fomu za kugombea nafasi hiyo.
Bi. Anjela ametoa wito kwa wanawake wengine wenye nia ya kugombea nafasi hiyo kujitokeza kwa wingi ili kuendelea kuleta usawa wa kijinsia katika uongozi na kutoa mchango wao kwa maendeleo ya Mkoa wa Manyara.
Phabiola Bohay ni mtoto wa mfanyabiashara tajiri anayemiliki kampuni ya mabasi maarufu ya Bashnet Coach, yanayofanya safari kati ya Babati na Mbulu.
Zoezi la kuchukua na kurejesha fomu linaendelea katika ofisi za UWT Mkoa wa Manyara.
0 Comments