F ‎BAWASA walipa bili ya Milioni 247 – Wapokea cheti cha pongezi kutoka TANESCO | Muungwana BLOG

‎BAWASA walipa bili ya Milioni 247 – Wapokea cheti cha pongezi kutoka TANESCO


Na John Walter -Babati 

‎Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Babati (BAWASA), chini ya uongozi madhubuti wa Mkurugenzi Mhandisi Iddy Yazid Msuya, imepokea Cheti cha Utambuzi wa Mchango na Ushirikiano wa Mteja kutoka kwa Meneja wa TANESCO Mkoa wa Manyara, Mhandisi Jahulula M. Jahulula.

‎Hii imekuja baada ya BAWASA kulipa deni la bili ya umeme lililofikia jumla ya Shilingi Milioni 247 (TZS 247,000,000).

‎Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa BAWASA, Mha. Iddy Yazid Msuya, deni hilo lilikuwa ni la nyuma, likihusiana na huduma za umeme katika Mamlaka ya Maji Orkesumet wilayani Simanjiro, ambayo nayo inahudumiwa na BAWASA.

‎Hatua hiyo imepongezwa na TANESCO kama mfano wa uwajibikaji na ushirikiano bora wa kibiashara kati ya taasisi za umma.

‎Kupitia taarifa yao, BAWASA imetoa shukrani za dhati kwa TANESCO Mkoa wa Manyara kwa kuthamini na kutambua mchango wao, huku ikisisitiza kwamba cheti hicho ni ishara ya wazi ya kuendelea kuimarisha mahusiano ya muda mrefu na ushirikiano wa kimaendeleo.

‎Aidha, BAWASA imeendelea kujipambanua kama taasisi inayotekeleza majukumu yake kwa weledi, uwajibikaji na uadilifu wa hali ya juu.

‎Pongezi maalum zimeelekezwa kwa timu nzima ya BAWASA, chini ya menejimenti imara na uongozi wa Mkurugenzi Mha. Iddy Yazid Msuya, kwa kujituma na kuonesha dhamira ya kweli katika kuhakikisha huduma bora za maji safi na usafi wa mazingira kwa wakazi wa Babati na maeneo jirani.

Post a Comment

0 Comments