F CDE Novat: Tutaipa Kilolo Thamani Kupitia Miradi ya Maendeleo | Muungwana BLOG

CDE Novat: Tutaipa Kilolo Thamani Kupitia Miradi ya Maendeleo


CDE Novat A. Mfalamagoha, kada wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), ameweka wazi dhamira yake ya kugombea nafasi ya Ubunge katika Jimbo la Kilolo mkoani Iringa, huku akisisitiza umuhimu wa matumizi sahihi ya fedha na rasilimali kwa maendeleo endelevu ya kiuchumi na kijamii kwa wananchi wa Kilolo.

Aidha, alisisitiza kuwa Kilolo ina rasilimali nyingi zikiwemo ardhi yenye rutuba, misitu, mito na vivutio vya utalii ambavyo bado havijatumiwa ipasavyo kuleta tija kwa wananchi. Aliahidi kuwa akichaguliwa kuwa Mbunge, atahakikisha rasilimali hizo zinatumika kama nyenzo muhimu za kukuza biashara ndogondogo, sekta ya kilimo na ufugaji, pamoja na kuibua fursa za ajira kwa vijana na wanawake.

Post a Comment

0 Comments