F Kijana Ajinyonga Kando ya Mto Erri, Babati. | Muungwana BLOG

Kijana Ajinyonga Kando ya Mto Erri, Babati.


Na John Walter-Babati

Kijana mmoja aliyetambulika kwa jina la James Mathayo, anayekadiriwa kuwa na umri wa kati ya miaka 27 hadi 28, amekutwa amejinyonga kwa kutumia kamba na kufariki dunia kando ya Mto Erri, katika Kijiji cha Erri, Kata ya Kiru, Wilaya ya Babati, mkoani Manyara.

Akithibitisha tukio hilo, Mwenyekiti wa Kijiji cha Erri, Ezekiel Mahu, amesema mwili wa kijana huyo ulikutwa ukining’inia karibu na mto huo, huku akiwa ameacha ujumbe katika simu yake sehemu ya rasimu (draft) uliosomeka: "kwenye kifo changu asihusishwe mtu yeyote."

“Kijana huyu alikuwa anaishi mjini Babati, lakini ni mkazi wa hapa kijijini, tukio hili limetushtua sana kama jamii,” amesema Mahu.

Taarifa zinaeleza kuwa James Mathayo ameacha mke na watoto, ingawa haijafahamika bado idadi kamili ya watoto wake.

Tukio hilo linatokea katika kipindi ambacho jamii ya kijiji hicho bado haijatulia kutokana na tukio la awali la kusikitisha ambapo mtoto wa kike mwenye umri wa miaka minne, Febronia Edward, alisombwa na maji ya mto huo wiki mbili zilizopita na hadi sasa hajapatikana.

Post a Comment

0 Comments