Na John Walter -Mbulu
Kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa mwaka 2025, Ismail Ussi, ametangaza kuridhishwa na miradi yote iliyokaguliwa katika Halmashauri ya Mji wa Mbulu, mkoani Manyara, na kusema kuwa miradi hiyo ina viwango vinavyotakiwa na inatekelezwa kwa ubora unaokusudiwa.
Akizungumza wakati wa kufunga mbio hizo katika mji huo, Ismail Ussi amewahimiza wananchi wote kujitokeza kwa wingi kutimiza takwa la kisheria na haki yao ya msingi ya kupiga kura kwenye uchaguzi mkuu wa Madiwani, Wabunge na Rais utakaofanyika Oktoba mwaka huu.
Kauli mbiu ya mwaka huu inasema: "Jitokeze kushiriki uchaguzi mkuu wa mwaka 2025 kwa amani na utulivu."
Kwa upande wake, Mkuu wa wilaya ya Mbulu, Michael Semindu, amesema Mwenge wa Uhuru mwaka huu unapitia na kuzindua jumla ya miradi 14 yenye thamani ya Shilingi bilioni 44, miradi ambayo inalenga kuboresha huduma za kijamii na kuinua uchumi wa wananchi wa Mbulu.
Mwenge wa Uhuru unaendelea na mbio zake katika maeneo mkoa wa Manyara huku ukiwa na dhamira ya kuhamasisha amani, umoja na maendeleo endelevu kwa Watanzania wote pamoja na kushiri katika uchaguzi mkuu wa mwaka huu.
Picha mbalimbali
0 Comments