F Miradi ya bilioni 9 kutembelewa na Mwenge wilayani Hanang'. | Muungwana BLOG

Miradi ya bilioni 9 kutembelewa na Mwenge wilayani Hanang'.


Na John Walter-Hanang'

Mwenge wa Uhuru umeingia rasmi katika Wilaya ya Hanang leo Julai 18, 2025, ukitokea Wilaya ya Mbulu, ukiendelea na mbio zake za kitaifa kwa mwaka huu.

Katika mapokezi rasmi, Mkuu wa Wilaya ya Hanang, Mheshimiwa Almish Hazal, alieleza kuwa mwenge huo utatembelea, utakagua, kufungua na kuweka mawe ya msingi kwenye jumla ya miradi nane yenye thamani ya shilingi bilioni 9.6.

Kauli mbiu ya mwaka huu ni: "Jitokeze Kushiriki Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2025 kwa Amani na Utulivu", kauli ambayo inalenga kuhamasisha wananchi kujitokeza kwa wingi kushiriki uchaguzi kwa njia ya kidemokrasia na kwa kudumisha amani.

Kabala ya kuwasili Hanang, Mwenge wa Uhuru ulikuwa Wilaya ya Mbulu ambapo ulipitia miradi 14 yenye thamani ya shilingi bilioni 44, ikiwemo miradi ya maendeleo ya kijamii, elimu, afya, maji na miundombinu.

Mwenge wa Uhuru mwaka huu unalenga kuhamasisha maendeleo ya wananchi, uwajibikaji wa viongozi, na kushiriki kwa wananchi katika miradi ya maendeleo sambamba na maandalizi ya uchaguzi mkuu ujao.

Post a Comment

0 Comments