Na John Walter -Simanjiro
Mwenge wa Uhuru ukiwa wilayani Simanjiro umekimbizwa umbali wa kilomita 159 na kuzindua, kukagua na kuweka mawe ya msingi kwenye miradi saba yenye thamani ya shilingi bilioni 6.1.
Miradi yote hiyo imepata kuridhiwa na kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru mwaka 2025, Ismail Ussi Fakii Lulandala.
Mkuu wa wilaya ya Simanjiro, akitoa taarifa kwa kiongozi huyo, amesema maelekezo yaliyotolewa yatafanyiwa kazi na kutekelezwa kwa wakati ili kuhakikisha manufaa ya miradi hiyo yanafika kwa wananchi.
Kuhusu afya, imeelezwa kuwa jumla ya watu 113 walipimwa virusi vya UKIMWI wakiwemo wanawake 24 na wanaume 89, ambapo mwanaume mmoja alikutwa na maambukizi.
Vilevile, watu 37 walipimwa malaria na hakuna aliyeonekana na ugonjwa huo, huku watu 14 wakijitolea kuchangia damu kwa hiari.
Mwenge wa Uhuru unaendelea na mbio zake mkoani Manyara ukiwa na kaulimbiu "tujitokeze kushiriki uchaguzi mkuu kwa amani na utulivu"
0 Comments