NA REBECA DUWE TANGA
Mkuu wa mkoa wa Tanga Balozi Dkt.Batilda Burian amewataka wananchi wa Mkoa wa Tanga wote kuachana na siasa za uchochezi bali waendelee kuilinda amani ya nchi kipindi hiki cha kuekea uchaguzi kwa kuiheshimu Sera ya kila Chama.
Mkuu wa mkoa wa Tanga aliyasema hayo wakati akizungumza katika kongamano la wafanyabiashara wadogowadogo yaliyofanyika katika ukumbi wa shule ya sekondari Tanga ufundi mkoani Tanga a bapo alitumia fursa hiyo kuwaasa wananchi wasiwe na maneno matusi kwa Chama chochote cha siasa.
"msimtukane mtu yeyote wala msing'oe bendera ya chama chochote badala yake msikilize Sera za kila Chama kwa utulivu bila kuathiri amani ya nchi yetu,waacheni wanadi Sera zao''alisema Balozi Dkt.Batilda Burian.
Aidha aliwahimiza kuangalia fursa kubwakubwa kwa kubuni mbinu za kiunua uchumi wao wenyewe na wa taifa kwa ujumla lakini pia waone namna gani ya kuboresha biashara zao ili wafikie kiwango kinachotakiwa.
"Changamoto zenu nimezichukua na nitazifanyia kazi hivyo muendelee kutoa ushirikiano kwa serikali yenu sikivu kwani Nia ya serikali ni kuwawezesha wafanyabishara waweze kufikia malengo yenu' alisema Balozi Dkt Buriani.
kwa upande wake katibu wa wafanya biashara Bi.Fatuma Ngoda ambaye pia ni mfanyabiashara wa biashara mbalimbali aliipongeza juhudi za serikali ya awamu ya sita ambayo imeweza kuwaunganisha wafanyabiashara wadogowadogo kuunda Chama hucho kilichoitwa Shiuma.
Aidha alisema kuwa zipo changamoto mbalimbali ikiwemo ukosefu wa mitaji ya kutosha miundo mbinu mbovu ya msoko na maeneo ya kuvanyia biasha elimu duni ya namna ya kuendesha biashara zao.
sambamba na hayo ameiomba serikali kuendelea kutoa mikopo kwa ajili ya kuboresha biashara zao lakini pia kuendelsa kuinua uchumi wa wafanya biashara wadogowadogo na nchi kwa ujumla.
Awali akisoma risala katika kongamano hilo afisa maendeleo jamiii mkoa wa Tanga Glori Maleo alisema kuwa serikali ya awamu ya sita imeanzisha mfumo wa kuwasajili wafanyabiashara wadogowadogo ili kuwatambua wafanyabiashara hao.
Alisema mpaka sasa katika mkoa wa tanga wamesajili watu 5825 kwa ujumla katika mkoa mzima wa Tanga,hata hivyo wamegawa vitambulisho 2124 ambapo pia wamegundua kuwa ipo haja ya kutoa elimu kwa wafanyabiashara hao ili waone umuhimu wa kujisajili kwa njia ya kielektroniki.



