Na John Walter-Karatu
Vijana wa mji wa Karatu wanaojishughulisha na usafirishaji abiria kutumia pikipiki maarufu kama "Bodaboda" wameonesha utayari wao wa kumpigia kura mgombea Urais wa Chama Cha Mapinduzi - CCM ili aweze kutekeleza ahadi yake ya kutenga fedha kwa ajili wafanyabiashara ndogo ndogo na bima ya afya kwa wote.
Wakizungumza mbele ya aliyekuwa mbunge wa viti maalum mkoa Arusha Cecilia Daniel Paresso ambaye ameamua kuingia mtaa kwa mtaa kumtafutia kura mgombea Urais wa CCM Dkt Samia Suluhu Hassan, vijana hao wamesema wamevutiwa na sera ya mikopo bila riba inayotolewa na serikali kupitia halmashauri kwa makundi maalumu ya vijana, wanawake na wenye ulemavu.
Pamoja na utayari wao kumuunga mkono Mgombea Urais wa chama cha mapinduzi CCM Dkt Samia Suluhu Hassan, vijana hao wameomba kuondolewa kwa kikwazo cha ukomo wa umri kwa wanaume katika mikopo ya bila riba inayotolewa na serikali kupitia halmashauri.
Kwa sasa mikopo isiyo na riba inayotolewa na serikali kupitia halmashauri imeweka huku huku wakisubiri kwa hamu ahadi ya bima ya afya kwa wote.
Kwa upande wake Cecilia Daniel Paresso mwenye ushawishi miongoni mwa vijana na wanawake katika jimbo la Karatu amewataka vijana hak kujitokeza kwenye mikutano ya kampeni ili wajue sifa ya kiongozi wa kumpigia kura Oktoba 29 mwaka huu.
Amewasihi vijana kumchagua mgombea Urais wa CCM Dkt Samia Suluhu Hassan ili aweze kutekeleza ahadi yake ya bima ya afya kwa wote itakayowanufaisha vijana wakimo wa bodaboda.
Wakati huu wa kampeni, wananchi wanahimizwa kwenda kusikiliza sera za wagombea wa vyama mbalimbali vya siasa ili wajue wa kumpigia kura Oktoba 29 mwaka huu.
