F CCM yazindua kampeni kwa kishindo Tarime Mjini | Muungwana BLOG

CCM yazindua kampeni kwa kishindo Tarime Mjini



NA Timothy Itembe Tarime.

UZINDUZI WA kampeni za uchaguzi wa Chama Cha mapinduzi Jimbo la Tarime mjini 2025 wazinduliwa Kwa mbwembwe mavuvuzela yatawala.

MJUMBE wa halmashauri kuu ya Chama Cha mapinduzi Taifa Joseph Kasheku Musukuma amemwagiza sifa Mgombea ubunge Jimbo la Tarime mjini Esther Matiko wakati akimombea kura kwenye uzinduzi wa kampeni uliofanyika uwanja wa Moira wa miguu maradufu shamba la Bibi.

Musukuma alisema anamfahami Esther kuwa ni jembe na Vikao vya uteuzi havikufanyakosa kumteuwa kuwa Mgombea ubunge Jimbo la Tarime mjini ambapo alimtaka Mgombea huyo kuanzia alipishia Mbunge mstaafu Michael Kembaki.

Naomba kura Kwa DKT Samia Suluhu Hassani na nafasi ya Ubunge naomba kura Kwa Esther Matiko pamoja na madiwani wanaotokana na Chama Cha mapinduzi alisema Musukuma.

Musukuma alitumia nafasi hiyo kuwananga Wanachama Cha upinzani kuwa wanapenda kupiga kelele lakini waliopo pewa magari ya kampeni hakuna aliye kataa kuchukua.

Naye Mgombea ubunge Jimbo la Tarime mjini,Esther Matiko alisema serikali imetekeleza miradi mingi ya maendeleo makubwa jambo ambalo limemsukuma kutimkuia Chama Cha mapinduzi.

Mbunge mstaafu na meneja kampeni, Michael Kembaki alisema nimekuja Kwa makusudi kabisa kuwambia kazi kubwa ambayo imefanywa na Rais wetu Mama Samia Suluhu Hassani Okotoba tumpe kura nyingi kama kukipa fadhila na siku hiyo hiyo tumpe kura nyingi Mgombea ubunge Jimbo la Tarime mjini aliyeteuliwa Esther Matiko hapa tupo Sabasaba tunasikia Kuna mjini Moja anaotwa wa ACT naomba mmpe kura za ndio RHaimondi Mwema ni mchapa kazi.

Pamoja na madiwani wote wanaotokana na Chama Cha mapinduzi wapeni wote kura bila kumsahau Mwalimu Matiko wa kata ya Kkenyamanyori tuqape kura za kutosha ili wawe madiwani na kuwatumikia.

"Naomba wastaafu wenzangu hususani madiwani kwanza aliyekuwa mwenyekiti wa halmashauri ya mji wa Tarime Daniel Komote na wengine jitokeze kuomba kura za Chama Cha mapinduzi Kwa wapiga kura ili kura zitoshe.na wagombea wa Chama Cha mapinduzi kushindwa"alisema Kembaki.

Kipindi hiki tathimini itatumika Kwa Jimbo ambalo litakuwa limetoa kura nyingi Kwa nafasi ya urais Ubunge  na Udiwani alisema mwenyekiti wa Chama Cha mapinduzi mkoa Mara,Patrick Chandi.

Mgombea Ubunge Jimbo la Tarime Vijijini Mwita Mwikwabe Waitara alisema mwaka 2020 tulisimama kwenye uwanja huu wa shamba la Bibi tukiomba kura Kwa Mgombea aliyekuwepo,Michael Kembaki na baada ya kupata kura miradi ilimiminika Jimbo la Tarime mjini mwaka huu msifamye kosa mpeni kura Esther Matiko ni mtu ambaye namjua.

Katika uchaguzi huu namuombea kura Mgombea Urais DKT Samia Suluhu Hassani na Mgombea Mwenza Balozi DKT Emmanuel Nchimbi na Kwa nafasi ya Ubunge Jimbo la Tarime mjini mpeni kura za kishindo Esther Matiko pamoja na madiwani wanaotokana na Chama Cha mapinduzi alisema Waitara.




Post a Comment

0 Comments