Na Timothy Itembe Tarime.
MKURUGENZI wa Chichake Sports Club Niclous Chichake amewakumbusha waandishi wa habari mkoa Mara kuandika habari za kuutangaza mkoa pamoja na vivutio vyake.
Chichake alisema hayo Jana alipoalikwa kuhudhuria na kutoa salamu Kwa mkutano mkuu wa dharura wa kilabu ya waandishi wa habari mkoa Mara ulioketi ukumbi wa hotel ya Gold Land ulioitoshwa na mwenyekiti wake Jacob Mugini wa kujadili maendeleo ya Kilabu.
"Tuone namna ya kuutangaza mkoa wetu na kujitangaza sisi wenyewe ili tuwe kivutio"ni ukweli usiopingika ukiemda kuangalia taarifa mnazoziandika ni ukweli mkoa wetu umefahamika na umetangazika ukiemda kuangalia Matiko mengi mnayoripoti matukio mengi yamekuwa ni ya maendeleo tofauti na hapo nyuma mengi yalikuwa ya migogoro"alisema chichake.
Madau huyo alisema waandishi wa habari mkoa Mara Kwa kipindi kifupi Kwa kuandika habari za maendeleo mkoani hapa zimebadili mtazamo na sura ya mkoa ambao sasa wawekezaji wameweza kuja kuwekeza Mara na Tarime ili kuinua uchumi.
Chichake alisisitiza pia kuwa Kuna haja waandishi kujiendeleza kielimu ili mwaandishi wa habari kufanikiwa kimaisha na anatamani kuona siku Moja mwaandishi kutoka mkoa Mara anaripotia vyombo vya kimataifa.
Kwa upande wake mwenyekiti wa kilabu ya waandishi wa habari mkoa Mara,Jacob Mugini alipongeza Mkurugenzi wa Chichake Sport Club kuwa karibu na kilabu ya waandishi Kwa malengo ya maendeleo.
Mwenyekiti alitumia nafasi hiyo kuteuwa wenyeviti wa kamati tatu za kilabu ya waandishi wa habari mkoa Mara Kwa Lengo la kuharakisha maendeleo ya Klabu ya Waandishi wa Habari Mkoa wa Mara na kuifanya kuwa klabu bora Tanzania
Karoli Jacob aliteuliwa kuwa mwenyekiti wa Kamati ya Mipango,Fedha na Mirad aliyeteuliwa
Kamati ya mambo ya Kijamii na Burudani ni Agribina Lucas na kamati ya Mafunzo ni Fresha kinasa.
0 Comments