F Kembaki awahakikishia CCM ushindi wa kishindo baada ya kuvunja makundi | Muungwana BLOG

Kembaki awahakikishia CCM ushindi wa kishindo baada ya kuvunja makundi



MBUNGE mstaafu wa Jimbo la Tarime mjini, Michael Kembaki amewahikishia ushindi wa kishindo wanachama wa Chama Cha mapinduzi baada ya kuvunja makundi yaliyokuwepo wakati wa kura za maoni na kuteuliwa Mgombea wa kupeperusha bendera ya Chama hicho,Esther Matiko.

Maamuzi ya kuvunja makundi yamekuja baada ya Mgombea mwenza wa Chama Cha mapinduzi Balozi DKT Emmanuel Nchimbi kufanya ziara wilayani Tarime na kumteuwa Michael Kembaki aliyeshinda kura za maoni kuwa kempena meneja wa Mgombea Ubunge aliyeteuliwa na Chama Jimbo la Tarime mjini Esther Matiko.

‎Wiki hii Mgombea mwenza wa Urais kupitia CCM Balozi Dkt Emmanuel Nchimbi alifanya ziara wilayani hapa katika miji ya Nyamongo na Tarime mjini na kuwataka wanachama wote kuvunja makundi na kuhakikisha wanaunga mkono wagombea walioteuliwa na chama hicho ambapo baada ya mkutano wa Nchimbi vikao vya Chama Cha mapinduzi ngazi ya wilaya Tarime kwa ajili ya kuvunja makundi viliketi ili kutekeleza maagizo yaliyotolewa.

Kikao Cha utekelezaji kilikaa na kuongozwa na mwenyekiti wake mkoa Mara,Patrick Chandi chini ya mjumbe wa NEC mkoa Mara Christopher Mwita Ghachuma pamoja na viongozi mbalimbali mkoa na wilaya ambapo kiliamua kwa Kauli Moja kuvunja makundi na kuletea Chama ushindi Katika uchaguzi unaotarajiwa kufanyika Okotoba 28,2024.

Mgombea Ubunge Jimbo la Tarime mjini,Esther Matiko alitumia nafasi hiyo kupongeza mwenyekiti wa Chama Cha mapinduzi Taifa na Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania DKT Samia Suluhu Hassani pamoja na Vikao vilivyo kaa na kumteuwa kuwa Mgombea ubunge Jimbo la Tarime mjini ambapo alimashukuru pia Michael Kembaki Kwa uamzi ambao amechukua wa kuvunja makundi kuwa ameonyesha ukomavu wa kisiasa.

"Baadhi ya watia nia wenzake akiwemo Michael Kembaki Hilsid Chambiri,Manchare Heche,Mussa Ryoba na wengine bila kubagua pamoja na wafanyabiashara wakubwa wakati na wadogo naomba waniunge mkono na kunipa kura za kutosha ili kuwatumikia nafasi ya Ubunge Jimbo la Tarime mjini sina mtu ambaye Nina mnyamyapaa hata kama ni Jack Kangoye ambaye emehamia Chama Cha upinzani ACT Wazalendo naomba kura za maoni alizopata zihamie kwangu"alisema Matiko.

‎‎Hata hivyo viongozi wa chama cha Mapinduzi wilayani hapa wametakiwa kuchukua hatua za kuunganisha wafanyabiashara na wanachama wa chama hicho ili kutafuta ushindi wa chama katika nafasi zote Urais Ubunge na Udiwani Kwa maana ya mafiga matatu alisema Matiko.

Matiko alipongenza Wanachama wa Chama Cha mapinduzi pamoja na baadhi ya wafanyabiashara kama vile mkurugenzi mtendaji wa kampuni ya kuuza mafuta ya magari PKM mkazi wa mji wa Nyamongo wa madini ya dhahabu,Kibiba Machage na wengine kushiriki harakati za kusaidia CCM kupata ushindi pamoja na kujitokeza mara kwa mara kutoa michango yao ya hali na mali muda wote.

Wakati huo huo wafanyabiashara wote wakubwa wakati na wadogo wilayani hapa na wazawa wote walio nje ya mkoa wa Mara wameombwa kushiriki kikamilifu kutafutia kura za chama cha mapinduzi na kuepuka kushiriki makundi ya kushika chama miguu na hivyo kusababisha kazi ya ushindi kuwa ngumu aliongeza Matiko.

‎Mmoja wa wafanyabishara wanaotajwa kushiriki kusaidia chama wilayani hapa Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya PKM ambaye ni mkazi wa Nyamongo na mjini Tarime,Kibiba Machage amekiri kuunga mkono Chama Cha mapinduzi Kwa kutoa nguvu zake pamoja na Mali zake Mara Kwa Mara kuhakikisha Chama kinasonga mbele na wakati huu wa uchaguzi Chama kinashinda Kwa kishindo na kuunda dola.

Mkurugenzi PKM Kibiba akiongea na waandishi wa habari kwanjia ya simu alipongeza ‎Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na mgombea urais kupitia CCM Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kusimamia vema vikao vya chama Taifa na kufanikisha kuteuliwa wagombea wanaokubalika akiwo Esther Matiko waJimbo la Tarime mjini na kusema yuko Tayari mda wote kusaidia Chama na wagombea wote Udiwani Ubunge na urais ili kupata ushindi.

viongozi wa chama hicho Kembaki alisema kuteuliwa Esther Matiko kuwa Mgombea ubunge Jimbo la Tarime mjini baada ya kura za maoni kupigwa na kuwa mshindi wa Tatu ni utaratibu wa Chama Cha mapinduzi na hakuna wa kukiuka maamuzi na mapendekezo ya Vikao vya ngazi ya juu

‎"Mimi kama kada wa CCM Ninaunga mkono mgombea wa Urais Samia Suluhu Hassan,mgombea ubunge Tarime Mjini Esther Matiko pamoja na wagombea wote wa CCM kata zote Tarime Mjini na Vijijini ili kuwezesha ushindi wa CCM katika uchaguzi mkuu wa mwaka huu"alisema.




Post a Comment

0 Comments