Njombe wapokea ugeni kutoka Shinyanga,Umaki CBWSO yawaeleza ilivyofanikia kutoa huduma ya maji

 








Jumuiya za watumia maji mkoani Njombe zimetakiwa kuacha kulimbikiza madeni ya bili za maji kwa taasisi za umma huku wakitakiwa kusitisha huduma hiyo ili ziweze kulipia huduma kama zinavyoweza kulipiwa kwa wakati huduma nyingine hali itakayopelekea uimara wa Jumuiya.


Wito huo umetolewa na ugeni maalum kutoka mkoa wa Shinyaga uliofika mkoani Njombe kwa lengo la kujifunza na kuzijengea uwezo CBWSO kutokana na mafanikio ambayo CBWSO nyingine zimefanikiwa katika uendeshaji.

Wakizungumza baada ya kujifunza namna UMAKI CBWSO ilivyofanikiwa kutoa huduma ya maji kwa kata tatu za Ukalawa,Matembwe pamoja na Kidegembye zilizopo wilaya ya Njombe John Singulile pamoja na Rashid Ngoy wakitokea mkoa wa Shinyanga wamesema licha ya mafanikio ambayo CBWSO za mkoa wa Njombe zimeyapata lakini bado kuna changamoto kubwa ya madeni limbikizi kutoka taasisi za serikali jambo ambalo linarudisha nyumba jumuiya zao.

"Ukiacha njia ya kuwakatia maji lakini njia nyingine rahisi kwa taasisi zenye kigugumizi kulipa ni kuzifungia mita za malipo kabla ya matumizi ya maji kama inavyofanyika kwenye umeme na hii itasaidia sana kuondoa madeni limbikizi"amesema John Singulile
 
Awali akitoa taarifa ya UMAKI CBWSO Meneja wa Jumuiya hiyo bwana Titus Udumbe amesema taasisi za Shule na Zahanati zimefikia deni la zaidi ya Milioni 40 "lakini kutokana na hili pia tumeona taasisi hizi zianze kuchangia huduma ya maji kupitia vifungu au wazazi kwa michango ya chakula ili watoto waendelee kupata huduma ya maji"amesema Udumbe

Nao maafisa Wakala wa Usambazaji maji na usafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA) Wilaya na mkoa wa Njombe akiwemo Richard Mwihava ambaye ni afisa maendeleo RUWASA wilaya ya Njombe wanasema ujio wa wageni hao umewafungua kwa kiasi kikubwa na kuziomba CBWSO kwenda kutumia ushauri walioupata ili kulipwa madeni.

Chapisha Maoni

Mpya zaidi Nzee zaidi