Wananchi Kisarawe waitwa Kambi ya madaktari bingwa Septemba 15


HALMASAHAURI ya Wilaya ya Kisarawe, mkoani Pwani, imewataka wananchi  wilayani humo kujitokeza kushiriki katika kambi maalumu ya  madaktari bingwa  inayotarajiwa kuanza Septemba 15 mwakaa.

Akizungumza, mkoani humo, juzi, Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Wilaya ya Kisarawe,  Yona Kabata, alisema  lengo la kambi hiyo ni kusaidia jamii inayoshindwa  gharama za kuwaona kwa wakati  madaktari bingwa wa  magonjwa mbalimbali.

Alisema kambi hiyo itakayo hitimishwa  Septemba 17 itahusu madaktari bingwa wa wanawake, mifupa, watoto, magonjwa ya ndani, koo, pua, masikio,mionzi na upasuaji.

 “Itakuwa ni kambi ya siku tatu, hivyo ninawaomba wananchi  wa Wilaya ya  Kisarawe kutumia fursa  hii muhimu kwa kujitokeza katika kambi hii,”alisema.

Alisema  wananchi watawaona madaktari bingwa bila malipo na kupewa huduma zote za kibingwa.

Dk. Kabata,alieleza  kambi hiyo itafanyika katika Hospitali ya Wilaya ya Kisarawe ambapo itawahusi wanchi wanao tumia kadi za Bima ya Afya na wasio tumia kadi hizo.

Alisema madaktari bingwa wanane wa Hospital ya Wilaya Kisarawe watatoa huduma za kibingwa kwa magonjwa  hayo ya wanawake, mifupa, koo, pua, masikio, upasuaji, mionzi na magonjwa ya ndani. 

“Wagonjwa wote wataofika na kubainika  kuwa na uhitaji wa huduma za zaidi watafanyiwa uchunguzi, upasuaji na ushauri,’alisema.

Dk. Kabata alieleza kambi  hiyo itakuwa kubwa kufanywa na madaktari bingwa wa hospitali hiyo mbali na  kliniki za kawaida wanazofanya.

“Hii inaashiria  kukua na kutanuka kwa  hudama za kibingwa na kuzosogeza karibu na  wananchi wanaoshindwa kumudu gharama za matibabu,”alisema.

Baadhi ya wanchi wilayani humo, wamepongeza uongozi wa  hospitali hiyo kwa kuandaa kambi hiyo ambapo wamedai itawasaidia kwa kiasi kikubwa kupata huduma za kibingwa kwa ukaribu  zaidi.

“Wakati mwingine ukifika hospitali  changamoto inakuwa ni kumwona daktari bingwa. Tunashukuru  uongozi wa Hospitali ya  Wilaya ya Kisarawe kwa kuletea huduma za kibingwa bure,”alisema  Husein Ali.



Chapisha Maoni

Mpya zaidi Nzee zaidi