Vijana zaidi ya 1000 Kunufaika na Mradi wa Kijana Togora


NA REBECCA DUWE TANGA

VIJANA zaidi ya Elfu moja wa Halmashauri ya jiji la Tanga Katika kata zote 27 wanatarajiwa kufikiwa na mradi wa kijana Togora tunakusikikza, unaotekelezwa na kampuni ya Afyacheck Chini ya Tanga Yetu ambao umelenga vijana wenye umri chini ya miaka 11 hadi 35 

Hayo aliyasema  Dr.Isaac Maro ambaye ni Mkurugenzi wa Afyacheck na msimamizi wa kijana Togora tunakusikiliza akizungumza katika uzinduzi wa mradi wa kijana Togora iliofanyika katika kituo Sanyansi stampark jijini Tanga, ambapo alisema kuwa baada ya utafiti  juu ya changamoto ya maisha ya vijana wa jiji la Tanga waliona  ni vyema kutengeneza utaratibu wa kuwasikiliza vijana ili kujua changamoto zao.

Samamba na hayo alisema kuwa vijana wanapaswa kuzungumza ili kujua changamoto wanazopitia katika maisha yo ili zipatiwe ufumbuzi ndio maana wameona kuanzisha huo mradi w kijana Togora  (togora )neno la kidigo linalomanisha kuzungumza .

"Mradi wa Kijana TOGORA: Tunakusikiliza unaotekelezwa na Taasisi ya AfyaCheck chini ya programu ya Tanga Yetu inayofadhiliwa na Botnar Foundation na kusimamiwa na Innovex. Mradi huu unalenga kusikiliza na kuwawezesha vijana kujadili kwa uwazi masuala yanayowagusa kwenye maeneo ya afya ya akili, afya ya uzazi na matumizi ya dawa za kulevya pamoja na vilevi.

Baada ya kuwasikiliza vijana Mradi huu pia umewaandalia programu mahususi ya kuwapatia suluhisho ya changamoto zao tajwa kwenye maeneo hayo matatu. Pongezi nyingi ziwaendee vijana wa Tanga  Jiji kwa kupewa jukwaa la kusikiliza sauti zao na hatimaye kuzitatua."alisema Maro

Aliongeza kusema lengo la mpango huo ni kuona namna gani wanaweza kumsaidia kijana kwani vijana wengi hawezi kuelezea  changamoto zao kwa wataalamu hivyo kupitia mradi huo wameweza kuleta namba maalumu ya Whatsap ambayo kijana atalezea shida yake na akapata ushauri wa kitaalumu.

Kwa upande wake Dkt Hasan Mshinda ambaye ni mwakilishi wa Botner foundation ambao ndio wafadhili wa miradi ya Tanga yetu ikiwemo Kijana Togora alisema kuwa katika utafiti waliouvanya waligundua awamu ya kwanza waliona matatizo mbalimbali ilikwemo mimba za utotoni ,maturities ya Madawa ya kulevya ambayo ndio hatarisha maisha ya vijana ambao ndio nguvu kazi Taifa  

Aidha alisema kuwa Mkoa wa Tanga upo kwenye ngazi ya juu kwa maturities ya Madawaska ya kulevya hivyo kupitia mpango huo wa kijana Togora tunakusikiliza watajua kwanini wanajihusisha matumizi hayo ya Madawa ya kulevya  kwamba watapa elimu ya jinsi ya kuachana uraibu huo ikiwemo ushirikiano katika ngazi ya familia .

Naye Mrakibu wa polisi wilaya ya Tanga Keneth Muhangwa alisema wao kama jeshi la polisi wameanzisha pia mradi wa ngorika kwa kuunga mkono juhudi hizo ili kutokomeza maturities ya Madawa ya kulevya  hivyo kwani mara nyingi wao wamekuwa wakidili na matokeo ya mambo yanayotoke katika jamii.

Kwa kuona hivyo tumeona  ni vyema sisi kama jeshi kuwa mradi mahususi kwa kudili utoaji wa elimu juu ya matumizi ya Madaya ya kulevya ambapo ni vyema kila kijana atoe ushirikiano ili kutimiza wajibu wake katika kutoa taarifa ya uhalifu na wahalifu badala ya kuhusika kuafanya uhalifu unaotokana matumizivya Madawa ya kulevya. 

Akizungumzi mradi huo Afisa maendeleo jiji la Tanga Bi.Fatma Kinyumbi ambaye ndiye alikuwa mgeni rasmi katika uzinduzi wa mradi huo uliofanyika katika  kituo cha sayansi Stampark iliyoko kisosora jijini Tanga aliwashukuru na kuwapongeza Botner faundation kwa miradi mbalimbali inayohusu vijana chini ya Tanga yetu.

"Mradi wa kijana Togora ni mradi Muhimu sana kwa vijana hivyo manapaswa  kuchangamkia fursa za elimu ili wafikie malengo yenu hususani kupitia mradi wa kijana Togora ni vyema kujitokeza kwa wingi ili kupata fursa inayotokana na mradi huo "alisema Kinyumbi.








Chapisha Maoni

Mpya zaidi Nzee zaidi