Mshindi wa bodaboda afya marathon apewa pikipiki na MATI


Na John Walter-Babati

Kampuni ya Mati Super Brands Ltd imetoa zawadi ya pikipiki kwa mshindi wa kwanza wa mashindano ya Bodaboda Afya Marathon, mbio za riadha za kilomita 10 kwa waendesha bodaboda, yaliyofanyika mjini Babati, mkoani Manyara na kuhitimishwa katika viwanja vya Tanzanite Kwaraa.

Mashindano hayo yameandaliwa na Rafiki Wildlife Foundation na kuzinduliwa na Mkuu wa Wilaya ya Babati, Mhe. Emmanuella Kaganda, kwa lengo la kuhamasisha waendesha bodaboda kujenga tabia ya kufanya mazoezi na kupima afya zao mara kwa mara, ili kuepuka magonjwa yanayoweza kusababishwa na mazingira ya kazi yao.

Akizungumza baada ya kukabidhi zawadi hiyo, Meneja Masoko wa Mati Super Brands Ltd mkoa wa Manyara, Present Temu, amesema kampuni hiyo imeamua kutoa pikipiki kama sehemu ya kurudisha kwa jamii na kuongeza motisha ya utendaji kazi kwa kundi la waendesha bodaboda, ambao wana mchango mkubwa katika sekta ya usafirishaji.

Kwa upande wake, Mkuu wa Wilaya ya Babati, Mhe. Emmanuella Kaganda, alitembelea na kukagua banda la Mati Super Brands Ltd na kupongeza uwekezaji wa kampuni hiyo katika uzalishaji wa vinywaji bora pamoja na mshikamano wao na jamii kupitia kushiriki matukio ya kijamii.

Washindi wa Bodaboda Afya Marathon 2025 ni:

Adam Yusuph – Zawadi pikipiki

Ibrahim Juma – Zawadi shilingi 500,000

Shaffi Iddi – Zawadi shilingi 400,000

Chapisha Maoni

Mpya zaidi Nzee zaidi